0
Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) amewataka watumishi wa Wizara ya Fedha na Mipango pamoja na Taasisi zake kuwahudumia wananchi kwa uadilifu ili kujenga uaminifu kwa wananchi na Serikali yao.

Dkt Mpango aliyasema hayo alipotembelea banda la Wizara ya Fedha na Mipango katika viwanja vya maonesho Nanenane katika eneo la Ngongo mkoani Lindi.

Alisema kuwa Wizara ya Fedha na Mipango inategemewa na wananchi wengi hivyo ni vyema wahudumiwe vizuripamoja na kutoa elimu kwa umma vya kutosha ili waweze kuelewa na kuridhika na huduma zinazotolewa na wizara.

“Tujitahidi kuwaelezea wananchi juu ya kazi na huduma zetu ili waweze kuzitumia kwa manufaa yao na Taifa kwa ujumla na tuweze kufikia uchumi wa viwanda kama lengo la Serikali ya Awamu ya Tano ilivyojipangia ” Alisisitiza Dkt. Mpango.

Kauli mbiu ya maonesho ya Nanenane mwaka huu ambayo ni ya 24 kufanyika kitaifa huku yakifanyika mwaka wan ne mfululizo mkoani Lindi inasema “Zalisha kwa tija mazao ya kilimo, mifugo na uvuvi ili kufikia uchumi wa kati”.

Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
Wizara ya Fedha na Mipango
Ngongo Lindi

Post a Comment

karibu kwa maoni

 
Top