Mwalimu
wa shule ya sekondari ya Nyakisasa iliyopo mkoani Kagera aliyetambulika
kwa majina ya Deogratias Simon anashikiliwa na jeshi la polisi Kagera
kwa tuhuma za kumkashfu Rais wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli.
Kamanda
wa polisi mkoa wa Kagera Augustine Ollom amesema kuwa mwalimu huyo
anashikiliwa kwa kosa la kutumia ukurasa wake wa Facebook kuikashfu
serikali na kumkashfu Rais Magufuli kuwa ni Dikteta na anaminya
demokrasia.
Aidha amesema kuwa kufutia hali hiyo tayari yupo mikononi mwa polisi na watakwenda naye mpaka dakika ya mwisho ili sheria iweze kutenda haki huku Kamanda amewaomba wananchi kuendelea kufichua watu wenye vitendo vya namna hiyo ili wawakabidhi polisi ili washughulikiwe

Post a Comment
karibu kwa maoni