0
Viongozi wa Dini nchini, wamesema Rais John Pombe Magufuli hajakataa kuonana na kuzungumza nao kama inavyoelezwa kwenye mitandao ya kijamii na baadhi ya vyombo vya habari.
 Hayo yamesemwa jana na Sheikh Mkuu wa Dar es Salaam, Alhad Mussa Salum ambapo alikanusha taarifazilizochapishwa na gazeti la Tanzania Daima la Septemba 21 ISSN 0856 9762 toleo namba 4310 na kusema kwamba taarifa hizo sio za kweli na zina nia ya kuchonganisha wananchi na viongozi wa dini na Rais Magufuli.
Na kuwaonya wasifanye hivyo, kwani Taifa ni letu sote. Aidha, Sheikh Mkuu ameeleza bayana kuwa nia ya viongozi hao kutaka kukutana na kuzungumza na Rais Magufuli ni kutokana na maono yao waliyoyapata kutoka kwa Mungu na sio kwamba wameagizwa na UKAWA.
Amesema kuwa tayari wameandika barua kwenda kwa Rais Magufuli ikiwa imesainiwa na Katibu Mkuu wa BAKWATA, Katibu Mkuu wa TEC na Katibu Mkuu wa CCT hivyo wanaamini kuwa Rais Magufuli ataafiki ombi lao.
 Ameeleza kuwa Rais Magufuli ni Rais makini, anawaheshimu viongozi wa Dini ndio maana kila mara huomba wananchi na viongozi wa dini wamuombee aweze kutekeleza majukumu yake.
 Hivyo amewasisitiza wananchi kupuuza uvumi wa aina yoyote unaoenezwa kuhusu mkutano wao na Rais.

Post a Comment

karibu kwa maoni

 
Top