0

Polisi wilayani  Geita mkoani Geita wametakiwa kuchunguza kifo cha kijana Chacha Gairige aliyeuawa kwenye mgodi wa Geita GGM  tarehe 20 septemba majira ya saa 11:30 na kuwakamata walinzi wa mgodi huo wa dhahabu wanaotuhumiwa kufanya mauaji hayo.

Chacha ni mkazi wa Geita na alikuwa mchimbaji mdogo wa madini ya dhahabu katika mgodi huo.

Kisa cha kuuawa kwake kinasemekana kuwa ni pale alipoingia katika machimbo hayo kuchukua mabaki ya madini [magwangala].I

Mkuu wa wilaya ya Geita Herman Kapufi ametaka uchunguzi ufanyike haraka na wahusika wachukuliwe hatua za kisheria.

Kwa mujibu wa rafiki yake Nelson Busumagu [18] mkazi wa Msufini mjini Geita ambaye walikuwa pamoja  siku hiyo anaeleza kuwa walinzi hao walimpiga jiwe kichwani kisha kumtumbukiza kwenye shimo lenye kina kirefu chenye  maji na mwili wake kuonekana ukielea ndani siku ya pili. 

Chacha aliuawa kikatili huku Nelson akijeruhiwa sehemu mablimbali za mwili wake.

Kamanda wa polisi mkoani Geita Mponjoli Mwabulambo amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kueleza kuwa waliuopoa mwili wa Chacha baada ya kuonekana ukiwa unaelea katika shimo lenye maji katika mgodi huo.

Post a Comment

karibu kwa maoni

 
Top