0
WANANCHI wa kata ya AYASANDA katika Halmashauri ya wilaya ya BABATI mkoani MANYARA wameishukuru Serikali kwa kuwajengea daraja
WANANCHI wa kata ya AYASANDA katika Halmashauri ya wilaya ya BABATI mkoani MANYARA wameishukuru Serikali kwa kuwajengea daraja linalounganisha kata yao na maeneo mengine wilayani humo.

Ujenzi wa daraja hilo uliogharimu zaidi ya shilingi milioni 430 unawawezesha wananchi wa Kata hiyo kusafiri na kusafirisha mazao yao kwa urahisi ikilinganishwa na siku za nyuma ambapo walikuwa wakipata usumbufu mkubwa.

Mara baada ya kuzinduliwa na Mmwenge wa uhuru daraja hilo, Kiongozi wa mbio za Mwenge wa uhuru kitaifa mwaka huu, GEOREGE MBIJIMA amewataka Wananchi wa eneo kulitunza daraja hilo kwa kuepuka kuharibu kingo za mto.

Post a Comment

karibu kwa maoni

 
Top