0
Licha ya elimu ya utunzaji wa mazingira na kutumia vyoo kutolewa kwa wananchi lakini bado imeonekana kuwa changamoto kubwa katika maeneo mengi hapa nchini.
Wako wengine wenye vyoo lakini matumizi yake sio mazuri,usafi haufanyiki na vingine havina ubora.
 
Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira LUHAGA MPINA.
 
Asilimia 43 ya Wakazi wa mkoa wa MANYARA haswa katika maeneo wanapoishi jamii ya wafugaji hawana vyoo hali inayowalazimu kujisaidia porini huku ikielezwa kuwa sababu ni Jamii hiyo  kubwa ya Wafugaji kuishi kwa kuhamahama kwa ajili ya kutafuta malisho ya mifugo yao.

Akitoa taarifa kwa Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira LUHAGA MPINA ambaye amefanya ziara mkoani MANYARA, Mkuu wa wilaya ya BABATI , RAYMOND MUSHI amesema kuwa ni asilimia 57 tu ya wakazi wa mkoa huo ndio wenye vyoo.

Kufuatia hali hiyo, Naibu Waziri MPINA ametoa muda wa  miezi mitatu kwa uongozi wa mkoa wa MANYARA kuhakikisha Wakazi wote  wa mkoa huo wanakuwa na vyoo.

Post a Comment

karibu kwa maoni

 
Top