Wakati vita
ya madawa ya kulevya ikiendelea hapa nchini,mkoa wa Manyara kupitia jeshi la
polisi limeanza operesheni kali ya kutafuta wahalifu mbalimbali wakiwemo watumiaji
wa madawa hayo na wauzaji.
Vita hiyo aliyoitangaza rais Magufuli na Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam kuanza nayo imeungwa mkono na watu wengi hapa nchi wakiwemo viongozi wa kidini.
Akizungumza
na waandishi wa habari katika ofisi za jeshi hilo mnadhimu [ACP] Longinus
A.Tibishubwamu amesema kuwa Operseheni hiyo ni endelevu na imeanza kwa
kuwakamata watu watatu wanaojihusisha na uuzaji na utumiaji wa bangi huku mmoja
akikutwa na coceine na wengine zaidi ya ishirini kwa kosa la uzururaji wakati
wa usiku.
Amewataja
waliokamatwa na madawa hayo kuwa ni Cecilia Alex maarufu kama Mama Chichi miaka
45 mkazi wa Osterbay Babati mjini [ misokoto 24 ya bangi] Issa Mstafa ambaye ni
fundi viatu mkazi wa Osterbay, miaka 27 hao ni wauzaji na watumiaji pamoja na Hemedi Ali, miaka 30 mkazi wa Komoto
aliekutwa na kete nne za madawa ya kulevya yanayodhaniwa kuwa ni Kokeini.
Aidha Tibishubwamu
ameeleza watu hao watafikishwa mahakamani kujibu mashtaka yanayo wakabili.
Kwaupande mwingine
akizungumzia swala laulinzi na usalama katika mkoa wa manyara unazidi
kuimarishwa zaidi ambapo kwa sasa wameeandaa kikosi maalumu kinacho fanya doria
usiku na mchana katika wilaya zote za Mkoa wa Manyara .
Kikosi hicho maalumu katika gari wanayoitumia imewekwa Rungu mbele na nembo iliyoandikwa kwa maandishi makubwa SIMBA DUME.
Post a Comment
karibu kwa maoni