Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi WILLIAM LUKUVI
Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi WILLIAM LUKUVI
amekutana na uongozi wa mikoa ya TANGA na MANYARA lengo likiwa ni
kumaliza mgogoro wa ardhi uliodumu kwa zaidi ya miaka kumi baina ya
wananchi wa wilaya ya KILINDI mkoani TANGA na KITETO mkoani MANYARA.
|
Mkuu wa mkoa wa Tanga Martine Shigel akizungumza katika mkutano huo. |
Waziri LUKUVI amesema wakati sasa umefika wa kumaliza tatizo hilo
hivyo kuwaomba viongozi wa mikoa yote miwili kutoa ushirikiano kwa
wataalamu watakaokwenda kuweka kuhakiki alama za mpaka.
|
Mkuu wa mkoa wa Manyara Dk. Joel Bendera akizungumza katika mkutano huo. |
Kwa upande wake mkuu wa mkoa wa Tanga MARTINE SHIGELA amesema
watahakikisha wanajipanga vizuri katika kutoa ushirikiano kwa wataamu wa
ardhi.
Naye mkuu wa mkoa wa Manyara JOEL BENDERA amewataka viongozi
walioshiriki kwenye kikao hicho kutobadili makubaliano ya awali ili
waweze kufikia lengo.
Katika kumaliza mgogoro huo serikali haitaweka mpaka mpya bali itazingatia tangazo la gazeti la serikali namba 95 la mwaka 1961.
Post a Comment
karibu kwa maoni