0
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwapungia mkono wananchi wa Kiteto alipoitembelea wilaya ya Kiteto.
Wilaya ya Kiteto Mkoani Manyara imeanza kutekeleza agizo la Waziri Mkuu Kassim Majaliwa la kuhakiki mashamba pamoja na kuvunja vitongoji vilivyoanzishwa kinyume cha sheria.

Waziri mkuu Majaliwa alitoa agizo hilo alipokuwa katika ziara yake Mkoani MANYARA lengo likiwa ni kukabiliana na migogoro ya ardhi mkoani humo.

Katika kutekeleza agizo hilo Mkuu wa wilaya ya Kiteto Mhandisi Tumaini Magessa ametembelea Vijiji vya Kimana, Pori Kwa Pori pamoja na Kijiji cha Kisima na kuzungumza na wananchi wa vijiji hivyo juu ya utekelezaji wa agizo la serikali la kuhakiki mashamba ili kuondoa migogoro ya ardhi inayoendelea katika wilaya hiyo.

Mkuu huyo wa Wilaya ya Kiteto amesema lengo la serikali kufanya uhakiki wa mashamba ni kuwabaini wamiliki hewa ambao waliyapata mashamba hayo bila kufuata utaratibu kutoka mamlaka za Serikali za Mitaa na Sheria za Ardhi.

Post a Comment

karibu kwa maoni

 
Top