0
Jeshi la polisi mkoa wa Dodoma limekamata shehena ya pombe kali za viroba zilizopigwa marufuku zenye thamani ya zaidi ya shilingi bilioni 1 kwa wakala mkuu wa uagizaji na usambazaji wa pombe hizo Dodoma Mselia Enterprises huku mmiliki wake Festo Mselia akijiua baada ya zoezi hilo kwa kujipiga risasi kichwani kwa kile kinachodaiwa ni msongo wa mawazo kutokana na mkopo aliochukua benki kwa ajili ya kuendesha biashara hiyo.

Msako huo wa pombe hizo zilizopigwa marufuku umeongozwa na kamanda wa polisi mkoa wa Dodoma Lazaro Mambosasa ambaye aliongozana na maofisa wengine wa jeshi hilo na kukuta zaidi ya katoni 1400 za viroba katika moja ya stoo za mfanyabiashara huyo na kufanya nae mahojiano na kisha kumtaka aendelee na shughuli zake na kisha kamanda huyo akaamuru shehena hiyo isiuzwe wala kutumika akisubiri maelekezo.

Kufuatia msako huo wa polisi ambao awali ulitanguliwa na maofisa wa mamlaka ya chakula na dawa nchini TFDA inadaiwa kuwa mfanyabishara huyo aliamua kujiua kwa kupiga risasi kichwani ambapo kabla ya umauti kumkuta kamera ya ITV ilinasa mazungumzo yake na maofisa wa TFDA akidai kuwa amesitisha uuzaji akisubiri maelekezo kutoka kwenye mamlaka husika kuhusu nini cha kufanya juu ya pombe hizo.

Kufuatia tukio hilo baadhi ya wakazi wa mkoa wa Dodoma wamekuwa na maoni tofauti kuhusu operation ya kuondoa pombe hizo ambapo wanasema licha ya kufanyika kwa nia ya kunusuru taifa na janga la ulevi lakini wangetoa muda kwa wafanyabishara kumaliza bidhaa zao kwani awali ilikuwa ikiendeshwa kihaliali ikiwemo kulipiwa kodi na tozo mbalimbali.

Katika tukio jingine jeshi hilo limefanikiwa kuwakamata wahamiaji haramu wanne raia wa Ethiopia na watanzania idadi kama hiyo ambao wanadaiwa kuhusika na  kuwa safirisha wahamiaji hao ambapo wote kwa pamoja wanatarajiwa kupandishwa mahakamani.

Post a Comment

karibu kwa maoni

 
Top