0
Mimi nilidhani utani mpaka  pale refariii alipopuliza kipenga kwamba mpira umekwisha lakini kumbe haikuwa utani ni mpira wa miguu ulikuwa ukiendelea uwanjani.
Arsenal walibomolewa na Bayern Munich kwa mara nyingine tena na kujikuta wakitolewa katika michuano ya Klabu Bingwa Ulaya katika ngazi ya timu 16 kwa kuzabwa jumla ya magoli 10-2.
Bayern MunichHaki miliki ya pichaREUTERS
Image captionRobert Lewandowski alifunga bao la kwanza
Arsene Wenger, ambaye atakuwa chini ya shinikizo kali kufuatia kichapo hiki, alishuhudia timu yake ikifungwa magoli 5-1, baada ya kuongoza kwa kupitia bao lililofungwa na Theo Walcott katika kipindi cha kwanza.
Mchezo ulibadilika baada ya Laurent Koschielny kumvuta Robert Lewandowski katika eneo la hatari na kusababisha penati, mapema kipindi cha pili. Koschienly pia alioneshwa kadi nyekundu baada ya mwamuzi kubadili mawazo kufuatia kumuonesha kadi ya manjano awali.
Baada ya hapo mafuriko yalianza, yakiongozwa na Arjen Robben, akifuatiwa na Douglas Costa na Arturo Vidal aliyefunga mabao mawili.
Real Madrid yatinga robo fainali
Katika mchezo mwingine wa ngazi ya timu 16, Sergio Ramos alipachika mabao mawili na kuipatia ushindi Real Madrid wa mabao 3-1 waliokuwa wakicheza ugenini dhidi ya Napoli.
Real MadridHaki miliki ya pichaFILIPPO MONTEFORTE
Image captionSergio Ramos alitikisa nyavu mara mbili
Vijana hao wa Zinedine Zidane walishinda kwa jumla ya mabao 6-2 na kujihakikishia nafasi ya kucheza robo fainali. Alvaro Morata alifunga bao la tatu la Real Madrid.

Post a Comment

karibu kwa maoni

 
Top