0
Mahakama ya Wilaya ya Hai Mkoani Kilimanjaro imetoa hukumu ya kuchwapwa kiboko kimoja mwanafunzi wa kidato cha tatu shule ya sekondari Longoi wilaya hapo baada ya kupatikana na hatia ya kumbaka na kumpa ujauzito mwanafunzi mwenzake wa shule hiyo

Akisoma hukumu hiyo Hakimu mkazi Mfawidhi wa mahakama hiyo, Agnes Muhina mbele ya mwendesha mashtaka wa polisi , Valeria Banda, alisema kuwa anatoa hukumu hiyo baada ya kuridhishwa na ushaidi uliotolewa mahakamani hapo usioacha shaka yoyote.

Kesi hiyo pia ilikuwa na mashahidi sita wa upande wa mashtaka akiwemo daktari wa hospitali ya Hai,dawati la jinsia na watoto na mama mzazi wa binti huyo, mwalimu na binti mwenyewe.

Ilidaiwa na mwendesha mashtaka wa polisi kuwa mtuhumiwa alitenda kosa hilo Oktoba 10, 2015 saa 8.00 mchana katika kijiji cha Mkalama Wilayani humo ambapo alimbaka na kumpa ujauzito mwanafunzi mwenzake wa kidato cha tatu mwenye umri (16).

Post a Comment

karibu kwa maoni

 
Top