0
Tangu mkuu wa mkoa wa Manyara Dk.Joel Bendera kutoa siku kumi na nne kuhakikisha mashamba yote yana hakikiwa hatimaye zimebaki siku 10 ili zoezi hilo liwe limeshatekelezwa.
Mkuu wa Mkoa wa manyara Dkt. Joel Bendera akiwa wilayani kiteto katika baraza la madiwani alitoa Siku 14 kwa Halmashauri ya Wilaya ya Kiteto kufanya uhakiki wa mashamba na maeneo yenye migogoro ya ardhi ili kumaliza migogoro hiyo.

Agizo hilo ni sehemu ya utekelezaji wa maagizo ya Waziri Mkuu Kassim Majaliwa alipokuwa mkoani Manyara.

Alisema kila mwenye shamba au eneo lenye mgogoro lazima lihakikiwe na mtu yeyote atakayebainika anamiliki shamba kinyume cha utaratibu sheria itachukua mkondo wake bila kujali umaarufu wala wadhifa wake.

Kwa upande wake Katibu Tawala wa Mkoa wa Manyara, Eliakim Maswi alisema migogoro mingi ya ardhi katika wilaya hiyo inasababishwa na baadhi ya viongozi wa Serikali za Vijiji.

Aidha Mkuu wa Wilaya ya Kiteto Mhandisi Tumaini Magesa amesema migogoro hiyo imesababishwa na watu kuchukua ardhi kubwa bila kufuata utaratibu.

Post a Comment

karibu kwa maoni

 
Top