0
JESHI la Polisi Kanda Maalum Dar es Salaam mnamo tarehe 8/04/2017 majira ya mbili usiku maeneo ya Tandale Uwanja wa Fisi lilifankiwa kumkamata mtu mmoja aliyefahamika kwa jina ka Paulo Baruti (38) mkazi wa Tandale kwa Mtogole akiwa amevaa sare za Jeshi la Polisi na kuwalazimisha wananchi waliokuwepo eneo hilo kumnunulia pombe la sivyo angewakamata na kuwafikisha kituo cha Polisi.
Katika Mahojiano hayo mtumiwa huyo alikiri kutumia sare hizo za Jeshi la Polisi kimakosa ambazo ni za kaka yake aitwaye Lyanga Baruti ambaye ni askari Polisi na sasa yupo likizo nyumbani kwao Mpanda mkoani Katavi.
Uchunguzi unaendelea ili kubaini kama mtuhumiwa huyo ni mara yake ya kwanza kufanya hivyo na kama pia hajawahi kushiriki katika matukio ya ujambazi kwa kutumia sare hizo.

Post a Comment

karibu kwa maoni

 
Top