0



Sakata la wasanii kutekwa mbunge wa jimbo la Momduli Julius Kalanga ameandika haya kwenye akauti yake ya facebook.
Julius Kalanga      
4 hrs

Mfumo huu wa utekaji na ukamataji usiozingatia sheria kwa raia wa nchi hii ni dalili ya wazi ya uwepo wa utawala wa kiimla usiozingatia haki za raia.
Ni wajibu wetu kuukataa kwa nguvu zote.
Freeroma mkatoliki.


Rapa Roma Mkatoliki ambaye hivi sasa anafanya vyema na wimbo wake 'Usimsahau mchizi' tangu amekamatwa na kupelekwa kusikojulikana na watu wasiojulikana naona bado kimya tuuu..

Imewagusa wasanii wengi na watanzania na wasio watanzania  wanajiuliza kulikoni mpaka watekwe?

Prof. Jay ameandika katika ukurasa wake wa Facebook kuwa Roma Mkatoliki, Moni Centrozone na kijana mmoja wa kazi walikamatwa jana wakiwa studio za Tongwe Records.

"Nimestushwa sana kusikia kuwa kuna watu wamevamia studio za Tongwe Records majira ya saa moja usiku na wamemchukua Roma, Moni na kijana wa kazi na pia wamechukua computer ya studio na Screen (Tv) na wameondoka navyo kusikojulikana. Mpaka sasa hatujui wamewapeleka wapi" aliandika Prof. Jay.





ROMA MKATOLIKI AMEKAMATWA USIKU HUU... Nimestushwa sana kusikia kuwa kuna watu wamevamia studio za TONGWE RECORDS majira ya saa moja usiku na wamemchukua ROMA @roma2030 , MONI@moni_centrozone na kijana wa Kazi na pia wamechukua COMPUTER ya studio na Screen (Tv) na wameondoka navyo kusikojulikana.. Mpaka sasa hatujui wamewapeleka wapi!!
Kwenye Facebook watu wameandika mengi zaidi wakihoji wapo wapi wasanii hao?
Tanzania Ehee
#WakinaRomawapoWapi
Aisee We pray for Them hayamambo tulikuwa tunaskiaga tu kwenye habari leo watu wanatoleana Bastola Mara kutekwa hii Ni dalili Mbaya kwa Nchi inayosifika kwa Amani.

Post a Comment

karibu kwa maoni

 
Top