YANGA yapiga hodi katika uongozi wa Azam FC kwa kutaka kumsajili beki wa kushoto Gadiel Michael ambae mkataba wake unafikia tamati mwenzi wa tisa mwaka huu.
Kiongozi mmoja ndani ya klabu ya Yanga ameithibitishia shaffidauda.co.tz kuwa klabu hiyo inahitaji saini ya beki huyo wa Azam na wanaangalia uwezekano wa kumsajili mara baada ya kumalizika kwa msimu huu kutokana na kiwango kikubwa alichoonyesha siku za hivi karibu.
Shaffidauda.co.tz. ilimtafuta Gadiel Michael kutaka kujua kama ana taarifa zozote kuhusiana mabingwa hao kutaka saini yake kwa ajili ya msimu ujao, ambapo alisema hana pingamizi la kutokujiunga na Yanga kama watafata taratibu zote na uongozi wake.
“Ligi ikifikia tamati ndiyo nitaanza kuzungumza na timu yoyote kama Azam bado hawajaniongezea mkataba lakini kwasasa mimi bado nina mkataba nao,” alisema Gadiel Michael.
Post a Comment
karibu kwa maoni