0
Mshauri wa Rais wa Nigeria Muhammadu Buhari, amelaani tendo hilo, ambalo amelitaja kuwa Haki miliki ya pichaFRSC RIVERS STATE/FACEBOOK
Image captionMshauri wa Rais wa Nigeria Muhammadu Buhari, amelaani tendo hilo, ambalo amelitaja kuwa "udunishaji wa wanawake"
Kamanda mkuu wa usalama barabarani Nigeria awakata nywele wafanyikazi wa kike
Shirika la kudhibiti usalama barabarani nchini Nigeria, limemuadhibu kamanda wake mmoja mkuu, baada ya kupigwa picha ya video akiwaadhibu wafanyikazi wa kike kwa kuwakata nywele zao ndefu.
Picha zinazoonyesha kamanda huyo wa kiume, akichukua mkasi na kuanza kuwakata wafanyikazi wa kike waliokuwa kwenye foleni ya kukaguliwa, iliwekwa mtandaoni, na sasa imesabisha malumbano makubwa sio tu nchini Nigeria bali kote Afrika na Duniani.
Kuna sheria inayodhibiti mtindo wa nywele kwa wafanyikazi wa kike kwenye kampuni ya kitaifa ya usalama barabarani- Federal Road Safety Corp (FRSC).
Bw Kumapayi akiwakata wanawake nywele za bandia mbele ya wenzaoHaki miliki ya pichaFRSC RIVERS STATE/FACEBOOK
Image captionBw Kumapayi akiwakata wanawake nywele za bandia mbele ya wenzao
Lakini msemaji amesema kuwa hatua ya kamanda huyo iko "nje ya" utendakazi wa FRSC.
Kwenye mtandao wa kijamii wa Twitter, Lauretta Onochie, mshauri wa Rais wa Nigeria Muhammadu Buhari, amelaani tendo hilo, ambalo amelitaja kuwa "udunishaji wa wanawake".
Andrew Kumapayi, kamanda mkuu wa kikanda wa FRSC katika jimbo la Rivers State, anasemekana alitekeleza adhabu mapema asubuhi wakati wa gwaride katika mji wa Port Harcourt siku ya Jumatatu.
Hajatoa maelezo yoyote.
Kiongozi mmoja wa wafanyikazi wa kike wa shirika hilo (FRSC), anasema kuwa wanafaa "kudumisha mtindo wa nywele ambao wanafaa kuingiza kwenye kofia zao za beret", lakini hakutaja marufuku ya kuwa na nywele ndefu.
Ameitwa katika makao makuu ili kuzomewa baada ya picha hizo kusambazwa mtandaoniHaki miliki ya pichaFRSC RIVERS STATE/FACEBOOK
Image captionAmeitwa katika makao makuu ili kuzomewa baada ya picha hizo kusambazwa mtandaoni
Picha kwenye mtandao wa Facebook kuhusiana na tendo hilo kwa sasa zimefutwa kutoka kwa mtandao rasmi wa shirika hilo, ingawa picha hizo zimesambazwa mara elfu katika mitandao ya kijamii.
Maandishi katika mtandao huo ulisema kuwa Bw Kumapayi, alikuwa akitekeleza ukaguzi wa "nywele, sare rasmi na makucha" kwa wafanyikazi.
Picha zimeonyeshwa za nywele zilizotapakaa ardhiniHaki miliki ya pichaFRSC RIVERS STATE/FACEBOOK
Image captionPicha zimeonyeshwa za nywele zilizotapakaa ardhini
Maafisa wengine waliohusika katika kisa hicho pia wameitwa katika makao makuu. Msemaji wa FRSC Bisi Kazeem, ameiambia shirika la habari la serikali ya Nigeria- NAN.
Uchunguzi unaendelea na "hatua kali itachukuliwa dhidi ya wote waliohusika" aliongeza.

Post a Comment

karibu kwa maoni

 
Top