0
Magufuli
Image captionMagufuli
Maelfu ya wafanyikazi wa serikali nchini Tanzania wamepatikana na vyeti bandia vya shule.
Kulingana na ripoti iliopokewa na rais Magufuli, takriban wafanyikazi 9,932 wa serikali wana vyeti ghushi vya shule.
Maelezo hayo yaliotolewa katika mji mkuu wa Dodoma yanaonyesha wafanyikazi 9,932 wa serikali walipatikana na vyeti bandia vya shule ya upili
Mwandishi wa BBC Sammy Awami anasema kuwa hiyo ni asilimia 2 ya wafanyikazi wote wa serikali wapatao 435,000.
Akizungumza baada ya kupata ripoti hiyo, rais Magufuli amewapatia maafisa walio na vyeti hivyo wiki chache za kujiuzulu la sivyo washitakiwe.
Pia ameyataka magazeti nchini humo kuchapisha majina ya maafisa hao.

Post a Comment

karibu kwa maoni

 
Top