0
nembo


JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA


WIZARA YA FEDHA NA MIPANGO


MUHTASARI WA HOTUBA YA WAZIRI WA FEDHA NA MIPANGO,
MHESHIMIWA DKT. PHILIP ISDOR MPANGO (MB),
AKIWASILISHA BUNGENI MAKADIRIO YA MAPATO NA
MATUMIZI YA WIZARA YA FEDHA NA MIPANGO
KWA MWAKA 2017/18











MEI, 2017
















Ukiuza toa risiti, Ukinunua dai risiti
Mhe. Dkt. John Pombe Joseph Magufuli, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
(13 Februari, 2016, Diamond Jubilee. Akiongea na Wazee wa Dar es Salaam)











  1. UTANGULIZI

  1. Mheshimiwa Spika, kutokana na taarifa iliyowasilishwa ndani ya Bunge lako Tukufu na Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Bajeti, naomba kutoa Hoja kwamba Bunge lako Tukufu, sasa lipokee na kujadili mapitio ya utekelezaji wa Mpango na Bajeti ya Wizara ya Fedha na Mipango kwa mwaka 2016/17  pamoja na Makadirio ya Mapato na Matumizi kwa mwaka  2017/18.

  1. Mheshimiwa Spika, awali ya yote naomba kumshukuru Mwenyezi Mungu, kwa kuniwezesha kusimama mbele ya Bunge hili kuwasilisha bajeti ya Wizara ya Fedha na Mipango kwa mwaka 2017/18.

  1. Mheshimiwa Spika, napenda nitumie fursa hii kumpongeza Mhe. Dkt. John Pombe Joseph Magufuli, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kuliongoza Taifa letu kwa malengo, ujasiri na uzalendo wa hali ya juu. Aidha, ninawapongeza Mhe. Samia Suluhu Hassan, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mhe. Kassim M. Majaliwa (Mb), Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kazi kubwa wanazofanya kwa dhati kumsaidia Rais katika utawala wa nchi yetu na kuwaletea maendeleo Watanzania wote. Mwenyezi Mungu azidi kuwapa afya njema, hekima na busara katika kuliongoza Taifa letu.

  1. Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2016/17, kumetokea matukio mbalimbali ambayo yamewagusa Watanzania. Katika kipindi hicho Bunge lako Tukufu lilipatwa na misiba ya kuondokewa na Waheshimiwa Wabunge wenzetu, Mheshimiwa Hafidh Ally Tahir aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Dimani - CCM na Mheshimiwa Dkt. Elly Marko Macha aliyekuwa Mbunge wa Viti Maalum-CHADEMA. Aidha, Taifa lilipata msiba mwingine wa aliyekuwa Spika Mstaafu wa Bunge la tisa Mheshimiwa Samwel John Sitta. Vile vile, Taifa lilipata maumivu makubwa kuondokewa na wanafunzi 32, walimu wawili na dereva mmoja wa shule ya Msingi ya Lucky Vicent kutokana na ajali iliyotokea Wilaya ya Karatu Mkoani Arusha tarehe 6 Mei, 2017. Aidha, Taifa lilipoteza askari polisi wanane (8) waliouawa katika kijiji cha Uchembe Kata ya Mjawa Tarafa ya Kibiti na vile vile wananchi ambao walikatishwa maisha kwa nyakati tofauti mwaka huu na kundi la kihalifu katika Wilaya ya Rufiji. Taifa letu pia limekumbwa na maafa ya mafuriko kutokana na mvua zilizokuwa zinaendelea kunyesha hususan katika mikoa ya Tanga, Morogoro, Dar es salaam pamoja na Zanzibar ambazo zilisababisha vifo, majeruhi pamoja na uharibifu mkubwa wa mali. Tunamwomba Mwenyezi Mungu aziweke roho za marehemu mahali pema peponi. Amina! na awaponye haraka majeruhi wote. Nitumie fursa hii pia kuwashukuru kwa dhati wale wote waliotoa misaada ya hali na mali kwa familia za wahanga wa matukio hayo.

  1. Mheshimiwa Spika, nitumie fursa hii kuwapongeza Wabunge wapya wa Bunge lako hili Tukufu walioapishwa hivi karibuni ambao ni Mhe. Abdallah Majura Bulembo (Mb.), Mhe. Anne Killango Malecela (Mb.), Mhe. Juma Ali Juma (Mb.), Mhe. Prof. Palamagamba John Aidan Mwaluko Kabudi (Mb.), Mhe. Salma Rashidi Kikwete (Mb.), Mhe. Dkt. Getrude Pangalile Rwakatare (Mb.) na Mhe. Catherine Nyakao Ruge (Mb.). Ninawapongeza sana na kuwakaribisha katika Bunge hili ili kwa pamoja tuweze kuwatumikia wananchi. Aidha, kwa namna ya pekee ninampongeza Mhe. Prof. Palamagamba John Aidan Mwaluko Kabudi (Mb.), kwa kuteuliwa kuwa Waziri wa Katiba na Sheria. Vivyo hivyo, ninampongeza Mhe. Dkt. Harrison George Mwakyembe Mbunge wa Kyela, kwa kukabidhiwa dhamana ya Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo.

  1. Mheshimiwa Spika, naomba pia kuchukua nafasi hii kukupongeza wewe, Naibu Spika na Wenyeviti wote wa Bunge kwa kuendesha majadiliano ya bajeti za Wizara mbalimbali kwa mwaka 2017/18 kwa mafanikio makubwa. Aidha, napenda kutambua mchango mkubwa na kumshukuru Mhe. Hawa Abdulrahman Ghasia, Mbunge wa Mtwara Vijijini na Mhe. Josephat Sinkamba Kandege, Mbunge wa Kalambo na Makamu Mwenyekiti kwa kuiongoza Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Bajeti kwa umakini. Natoa shukurani za dhati kwa wajumbe wote wa Kamati kwa maoni, ushauri na mapendekezo waliyotoa ili kuboresha Mpango na Bajeti ya Wizara ya Fedha na Mipango kwa Mwaka 2017/18.

  1. Mheshimiwa Spika, naomba pia nitoe shukurani zangu za dhati kwa Mheshimiwa Dkt. Ashatu Kachwamba Kijaji Mbunge wa Kondoa na Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, kwa ushirikiano na msaada anaonipatia katika  kuhakikisha utekelezaji wa majukumu ya Wizara yangu unafanikiwa. Aidha, nawashukuru Bw. Doto James (Katibu Mkuu na Mlipaji Mkuu wa Serikali), Naibu Makatibu Wakuu Bibi Dorothy S. Mwanyika, Bibi Amina Kh. Shaaban, Dkt. Khatibu M. Kazungu kwa kusimamia vema shughuli za kila siku za kiutendaji za Wizara yangu. Pia napenda kutoa shukurani zangu za dhati kwa Prof. Benno Ndulu - Gavana wa Benki Kuu, Ndg. Charles E. Kichere - Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania, Dkt. Oswald J. N. Mashindano - Msajili wa Hazina na Dkt. Albina Chuwa - Mtendaji Mkuu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu kwa kutekeleza majukumu ya kusimamia kwa weledi taasisi nyeti walizokabidhiwa.  Taasisi hizi zinatoa mchango mkubwa sana katika utekelezaji wa majukumu ya Wizara na maendeleo ya nchi kwa ujumla. Nawashukuru pia, Makamishna, Wakurugenzi, Wakuu wa Taasisi zote zilizoko chini ya Wizara, Wakuu wa Vitengo na wafanyakazi wote wa Wizara, kwa kutimiza wajibu wao vema wa kuwatumikia watanzania.
  1. Mheshimiwa Spika, baada ya utangulizi huo, yafuatayo ni maelezo ya majukumu ya Wizara katika  kujenga msingi wa uchumi imara, mapitio ya utekelezaji wa Mpango na Bajeti kwa Mwaka 2016/17 na malengo ya Mpango na Bajeti  kwa Mwaka 2017/18.

2.0 MAJUKUMU YA WIZARA KATIKA KUJENGA MSINGI WA UCHUMI IMARA

  1. Mheshimiwa Spika, mojawapo ya majukumu ya Wizara ni kujenga msingi wa uchumi imara ili kufanikisha jukumu hili ujenzi wa uchumi imara, bajeti hii imeandaliwa kwa kuzingatia yafuatayo: Ilani ya Uchaguzi ya CCM 2015-2020; Mpango wa Pili wa Maendeleo ya Taifa wa Miaka Mitano 2016/17-2020/21; Dira ya Maendeleo ya Taifa 2025; na Malengo ya Maendeleo Endelevu 2030. Lengo kuu la mpango na bajeti ya Wizara ni kutekeleza kauli mbiu ya Serikali ya Awamu ya Tano ya kujenga uchumi imara unaoongozwa na Sekta ya Viwanda. Ili kufikia lengo hili, Wizara ilijielekeza katika kuimarisha utulivu wa uchumi, usimamizi bora wa ukusanyaji wa mapato, kupanua wigo wa  kodi, kusimamia kwa umakini zaidi matumizi ya fedha za Umma na kuratibu utekelezaji wa Mipango ya Maendeleo ya Taifa.

  1. Mheshimiwa Spika, katika kujenga uchumi imara, Aidha, Wizara ikiongozwa na Sera ya Fedha ilijikita katika kuhakikisha kuwa kuna usimamizi wa malengo mapana ya kitaifa ya ukuaji wa uchumi, kudhibiti mfumuko wa bei, na mapato na matumizi ya Serikali. Katika mwaka 2016/17, Serikali ilikusudia kutimiza malengo yafuatayo: Kuongeza ukuaji wa Pato la Taifa kutoka asilimia 7.2 kwa mwaka 2016 hadi asilimia 7.3 mwaka 2017 na asilimia 7.4 kwa mwaka 2018; kuhakikisha mfumuko wa bei unabaki kwenye kiwango cha tarakimu moja; na kuhakikisha nakisi ya bajeti ya Serikali haizidi asilimia 4.5 ya Pato la Taifa.

  1. Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2016 ukuaji ulikua kwa uchumi wa wastani wa asilimia 7.0 katika mwaka 2016 na ulitokana na ukuaji wa kasi wa shughuli za kiuchumi katika sekta ya mawasiliano asilimia 13.0, sekta ya ujenzi asilimia 13.0, sekta ya usafirishaji na uhifadhi asilimia 11.8, pamoja na sekta ya madini na uchimbaji mawe ambayo ilikua kwa asilimia 11.5. Mchango mkubwa wa kiuchumi (katika GDP) kwa mwaka 2016 ulitokana na sekta ya ujenzi (asilimia 20.2), usafirishaji na uhifadhi (asilimia 10.8), biashara ya jumla na rejareja (asilimia 9.9), mawasiliano (asilimia 8.3) na uzalishaji viwandani (asilimia 8.2).

  1. Mheshimiwa Spika, utekelezaji thabiti wa Sera ya Fedha uliwezesha na juhudi zaidi katika ukusanyaji mapato ya Serikali na kusimamia matumizi ulisababisha kuwepo kwa utulivu wa thamani ya shilingi ya Tanzania dhidi ya dola ya Marekani.  ambapo dola 1 ya Marekani ilibadilishwa kwa wastani wa kati ya shilingi za Kitanzania 2,180 Juni 2016 na shilingi 2,220 Machi, 2017.  Aidha, mfumuko wa bei uliendelea kubakia kati ya 5.1% 20 July 2016 na 6.4% Machi, 2017 katika kipindi chote cha miezi tisa ya mwaka wa fedha 2016/17, ukiwa ndani ya ukomo wa asilimia 8.0 uliowekwa chini ya makubaliano ya nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki. Vile vile, mfumuko wa jumla wa bei ulipungua kutoka asilimia 5.5 mwezi Juni 2016 hadi asilimia 5.0 mwezi Desemba 2016. Mfumuko wa bei unatarajiwa kuendelea kubakia katika viwango vya tarakimu moja katika siku zijazo kutokana na kushuka kwa bei ya mafuta nchini inayotokana na utulivu wa bei ya mafuta katika soko la dunia na utulivu wa thamani ya shilingi.

3.0 MAPITIO YA UTEKELEZAJI WA MPANGO NA BAJETI YA WIZARA KWA MWAKA 2016/17

  1. Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2016/17, Wizara iliendelea kutekeleza majukumu yake kupitia mafungu tisa ya kibajeti na Taasisi na Mashirika yaliyo chini yake (Jedwali na.1). Mafungu hayo ni Fungu 50-Wizara ya Fedha na Mipango, Fungu 21-Hazina, Fungu 22-Deni la Taifa, Fungu 23-Idara ya Mhasibu Mkuu wa Serikali, Fungu 10-Tume ya Pamoja ya Fedha, Fungu 13-Kitengo cha Udhibiti wa Fedha Haramu, Fungu 7- Ofisi ya Msajili wa Hazina, Fungu 66-Tume ya Mipango na Fungu 45-Ofisi ya Taifa ya Ukaguzi.

  1. Mheshimiwa Spika, ili kufanikisha utekelezaji wa Sera za Uchumi Jumla, katika mwaka 2016/17, shughuli zilizopangwa kutekelezwa, mapato na matumizi ya Wizara ni kama inavyooneshwa kwenye kitabu cha hotuba hii kuanzia aya namba 14 hadi 18 (ukurasa namba 9-13).



3.4 UTEKELEZAJI WA MAJUKUMU KWA MWAKA 2016/17

  1. Mheshimiwa Spika, naomba sasa kulieleza Bunge lako Tukufu kuhusu utekelezaji wa majukumu na bajeti ya Wizara ya Fedha na Mipango kwa mwaka 2016/17.

3.4.1 Kubuni na kusimamia Utekelezaji wa Sera za Uchumi Jumla

  1. Mheshimiwa Spika, Wizara ya Fedha na Mipango ndiyo yenye jukumu la kusimamia na kuhakikisha Uchumi Jumla unakua na kuwanufaisha wananchi wote. Ili kufanikisha jukumu hili, Wizara imeendelea kuhakikisha sera za kukuza uchumi na kuondoa umasikini zinatungwa ili kusimamia sheria, kanuni na taratibu za fedha, Mapato na Matumizi ya fedha za Umma na Mipango ya Maendeleo ya Taifa. Sera ya Fedha inajumuisha viashiria vya mwenendo wa uchumi jumla kama vile: mfumuko wa bei, riba za mikopo na amana, thamani ya shilingi, akiba ya fedha za kigeni, na ujazi wa fedha na karadha. Sera ya Mapato na Matumizi inajumuisha mapato ya ndani (Kodi na mapato yasiyo ya kodi na mikopo ya ndani) na mapato ya nje (Misaada, mikopo yenye masharti nafuu na mikopo yenye masharti ya kibiashara). Kipengele cha matumizi kinajumuisha matumizi ya kawaida na matumizi ya maendeleo.

  1. Mheshimiwa Spika, pamoja na jukumu lake la msingi la kuandaa na kutekeleza sera za fedha na kibajeti zinazolenga kuwa na kiwango kidogo cha mfumuko wa bei kwa ajili ya ukuaji endelevu wa uchumi wa Taifa. Hadi kufikia Machi, 2017 kasi ya ukuaji wa uchumi imeendelea kuwa ya kuridhisha na kubakia katika wastani wa asilimia 7 kwa mwaka kwa kipindi cha miaka mitatu mfululizo.
3.4.2 Uratibu wa Mipango ya Maendeleo ya Taifa

  1. Mheshimiwa Spika, Wizara kupitia Tume ya Mipango imeendelea kusimamia utekelezaji wa Mipango ya Maendeleo na kutoa elimu kwa wadau kwa kutekeleza yafuatayo: kuchapisha na kusambaza nakala 10,000 za Kitabu cha Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa Miaka Mitano (2016/17-2020/21), kutoa elimu kwa Maafisa Mipango 185 kutoka Sekretarieti za Mikoa na Maafisa Mipango 237 kutoka Halmashauri kuhusu Mwongozo wa Uwekezaji wa Umma ili kuwajengea uwezo wa kutafsiri vipaumbele vya kitaifa katika mipango ya maendeleo katika maeneo yao; na kuchapisha na kusambaza kwa wadau nakala 930 za Mwongozo wa Usimamizi wa Uwekezaji wa Umma; na kutoa elimu ya Mwongozo huo. Aidha, Tume ya Mipango iliandaa na kuwasilisha Mapendekezo ya Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa mwaka 2017/18 katika mkutano wa Tano wa Bunge la 11, Novemba 2016.

  1. Mheshimiwa Spika,  Aidha, katika mwaka 2016/17 Wizara kupitia Tume ya Mipango, kwa kushirikiana na Wizara za Kisekta ilifanya ufuatiliaji wa miradi 42 ya Sekta ya Umma na binafsi hususan katika sekta ya viwanda, maji, kilimo, nishati na miundombinu katika mikoa ya Arusha, Dar es Salaam, Dodoma, Tabora, Mwanza, Kilimanjaro, Tanga, Pwani, Lindi na Mtwara. Taarifa ya ufuatiliaji huo imewezesha Wizara kubaini mafanikio na changamoto ambazo zimetumika kupanga hatua za kuchukua wakati wa utekelezaji wa Mpango wa Mwaka 2017/18.




3.4.3 Uratibu wa Mikakati ya Kupunguza Umasikini

  1. Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2016/17, Wizara iliendelea kuratibu jitihada za kupambana na umasikini nchini ikiwemo kuandaa Mpango wa Kitaifa wa Ufuatiliaji na Tathimini ya Hali ya Umasikini Nchini.  Aidha, Wizara kwa kushirikiana na Sekta mbalimbali inaendelea kukamilisha Taarifa ya Hali ya Umasikini Nchini. Takwimu zilizopo za viashiria vya umasikini nchini zinaonyesha kuwa kiwango cha umasikini ni asilimia 28.2 ikilinganishwa na asilimia 32 kwa mwaka 2007.  Hata hivyo, kiwango hiki bado ni kikubwa hasa vijijini (33.3%) na hakikubaliki.  Jitihada za Serikali kupambana na umasikini ni pamoja na kuongeza tija na thamani ya mauzo ya kilimo, mifugo, uvuvi, na shughuli nyingine za uchumi vijijini.  Kwa upande wa huduma za msingi za jamii viashiria vinaonyesha matokeo mazuri ya kutia moyo ikiwa pamoja na kupungua kwa vifo vya watoto wachanga chini ya mwaka mmoja, nyumba na makazi bora zaidi na kiwango cha upatikanaji maji safi na salama.  

  1. Mheshimiwa Spika, Wizara kwa kushirikiana na Ofisi ya Rais-TAMISEMI iliendesha mafunzo kwa Maafisa Maendeleo ya Jamii, Maafisa Ustawi wa Jamii, Maafisa Mipango na Wachumi kutoka idara mbalimbali za Halmashauri zote nchini kuhusu Malengo ya Maendeleo Endelevu na Hali ya Umasikini Nchini. Mafunzo hayo yalilenga kuelimisha na kukuza uelewa wa wataalam mbalimbali kwa lengo la kuchambua na kujumuisha malengo hayo katika mipango na bajeti katika mwaka 2017/18. Jumla ya Maafisa 427 kutoka Halmashauri 185 na Maafisa 52 kutoka Sekretarieti za Mikoa yote nchini walihudhuria.


  1. Mheshimiwa Spika, Wizara kwa kushirikiana na Shirika la Umoja wa Mataifa la Maendeleo (UNDP), Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na Taasisi ya Utafiti wa Uchumi na Jamii (Economic and Social Research Foundation -ESRF) pia, ilifanya tathmini ya miradi inayotekelezwa ili kuondoa umasikini na kutunza mazingira katika wilaya za Bunda (Mara), Sengerema (Mwanza), Bukoba (Kagera), Ikungi (Singida), Ileje (Mbeya) na Nyasa (Ruvuma). Miradi hii inayotekelezwa kwa ushirikiano kati ya Serikali na UNDP ni ufugaji wa samaki katika vizimba ndani ya Ziwa Victoria  na katika malambo nje ya ziwa, ufugaji wa nyuki kwa njia za kisasa na uzalishaji wa nishati mbadala (gesi) ya majumbani kwa kutumia samadi.

 3.4.4 Usimamizi wa Ukusanyaji wa Mapato ya Serikali
 
  1. Mapato ya Ndani

  1. Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2016/17, sera za mapato zililenga kukusanya mapato ya kodi na yasiyo ya kodi ya shilingi bilioni 17,798.10 (ikijumuisha mapato ya Mamlaka za Serikali za Mitaa). Hadi Aprili, 2017 jumla ya makusanyo ya ndani (ikijumuisha mapato ya Mamlaka za Serikali za Mitaa) yalikuwa shilingi bilioni 13,604.0 sawa na asilimia 76 ya makadirio. Kati ya kiasi hicho, mapato ya kodi yalifikia shilingi bilioni 11,644.6 sawa na asilimia 77 ya lengo la mwaka la kukusanya shilingi bilioni 15,105.1; mapato yasiyo ya kodi yalifikia shilingi bilioni 1,600.8 sawa na asilimia 79 ya lengo la mwaka la shilingi bilioni 2,027.6; na mapato ya Mamlaka ya Serikali za Mitaa yalikuwa shilingi bilioni 398.7 sawa na asilimia 60 ya lengo la kukusanya shilingi bilioni 665.4 kwa mwaka. Vile vile, mikopo kutoka vyanzo vya ndani ilifikia shilingi bilioni 4,715.7, sawa na asilimia 88 ya shilingi bilioni 5,374.30 zilizotarajiwa kukopwa kwa mwaka.  Matokeo hayo yanatokana na kuendelea kuwepo kwa changamoto ikiwa pamoja na ukwepaji kodi, wigo mdogo wa vyanzo vya mapato, udhaifu katika ukusanyaji na elimu ndogo kwa mlipa kodi.

  1. Mheshimiwa Spika, Wizara imeendelea kusimamia matumizi ya vifaa na mifumo ya kielektroniki katika ukusanyaji wa mapato ili kuongeza ufanisi na kudhibiti upotevu wa mapato; kupanua wigo wa walipa kodi ikiwa ni pamoja na kurasimisha sekta isiyo rasmi ili iweze kuingia katika mfumo wa kodi; kuimarisha ukusanyaji wa mapato yasiyo ya kodi na kuboresha usimamizi wake; kusimamia ulipaji ili kuongeza mapato yatokanayo na kodi ya majengo; na kuendelea kudhibiti na kupunguza misamaha ya kodi isiyo na tija. Aidha, Wizara imeendelea kuratibu mapendekezo ya wadau mbalimbali ya kuboresha sera za bajeti hususan mapato kupitia Kikosi Kazi cha Maboresho na kusimamia utekelezaji wa Sheria ya Fedha ya Mwaka 2016.

  1. Misaada na Mikopo nafuu toka kwa Washirika wa Maendeleo

  1. Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2016/17, Washirika wa Maendeleo waliahidi kuchangia Bajeti ya Serikali kiasi cha shilingi bilioni 3,600.8. Kati ya fedha hizo, Misaada na Mikopo nafuu ya Kibajeti (GBS) ni shilingi bilioni 483, mifuko ya kisekta ni shilingi bilioni 372.1 na miradi ya maendeleo ni shilingi bilioni 2,745.7.

  1. Mheshimiwa Spika, hadi kufikia Aprili, 2017 Serikali imepokea kiasi cha shilingi bilioni 2,340.1 sawa na asilimia 65 ya lengo la mwaka. Kati ya kiasi kilichopokelewa, shilingi bilioni 111.4 ni Misaada na Mikopo nafuu ya Kibajeti (GBS) sawa na asilimia 23 ya ahadi  ya mwaka, shilingi bilioni 324.4 ni za mifuko ya pamoja ya kisekta sawa na asilimia 87 na shilingi bilioni 1,904.3 kwa ajili ya Miradi ya Maendeleo sawa na asilimia 69 ya lengo la mwaka.
  2. Mheshimiwa Spika, kuchelewa kupatikana kwa fedha za Washirika wa Maendeleo kunatokana na sababu mbalimbali zikiwemo: kuchelewa kukamilika kwa vigezo na taratibu za kutoa fedha tofauti na ilivyokusudiwa kwa baadhi ya Washirika wa Maendeleo; taratibu za majadiliano kutokamilika kwa wakati; Uthamini wa mali na ulipaji wa fidia kwa miradi mikubwa kuchukua muda mrefu na hivyo kuathiri utoaji wa fedha; na  kasi ndogo ya utekelezaji wa baadhi ya miradi ya kisekta  ambayo husababisha Washirika wa Maendeleo kuchelewa kutoa fedha kwa ajili ya utekelezaji wa miradi husika.

  1.     Mheshimiwa Spika,  mwenendo huu wa upatikanaji wa mapato ya Serikali (mapato ya ndani, misaada na mikopo nafuu) umesababisha utoaji wa fedha kwa ajili ya matumizi ya kawaida na matumizi ya maendeleo kuwa chini ya matarajio.  Fedha zilizotolewa hadi Machi 2017 ni Tshs. 14.0 trillioni matumizi ya kawaida (79.2% ya lengo la Tshs 17.9 trilioni) na Tshs. 5.0 trilion (42.5% ya lengo la 11.8 trilioni).

3.4.5 Uandaaji na Usimamizi wa Utekelezaji wa Bajeti ya Serikali

  1. Mheshimiwa Spika, katika utekelezaji wa Bajeti ya Serikali ya mwaka 2016/17, Wizara ilitekeleza yafuatayo: kuandaa, kuchapisha na kusambaza Mwongozo wa Maandalizi ya Mpango na Bajeti wa Mwaka 2017/18 kwa Wizara, Idara zinazojitegemea, Wakala, Taasisi, Sekretarieti za Mikoa na Mamlaka za Serikali za Mitaa; Vitabu vya Makisio ya Bajeti ya Serikali kwa mwaka 2017/18 (Juzuu Na. I, II, III na IV) na kuviwasilisha Bungeni kwa ajili ya kujadiliwa; na kijitabu cha Bajeti ya Serikali ya mwaka 2016/17 toleo la Wananchi (Citizen Budget). Aidha, Wizara ilivifanyia marekebisho na kuchapisha Vitabu vya Makisio ya Bajeti ya Serikali kwa mwaka 2016/17 (Juzuu Na. I, II, III na IV) kama ilivyoidhinishwa na Bunge.

  1. Mheshimiwa Spika, katika kuhakikisha Bajeti ya Serikali inasimamiwa na kutekelezwa kwa mujibu wa Sheria, Wizara iliandaa: Waraka wa Hazina Na.1 wa Utekelezaji wa Bajeti wa Mwaka 2016/17, Mwongozo wa Mafunzo ya Sheria ya Bajeti Na. 11 ya Mwaka 2015, Kijitabu kinachofafanua Sheria ya Bajeti na kuendesha mafunzo ya Sheria ya Bajeti kwa Maofisa 187 kutoka kwa Wakala, Taasisi na Mashirika ya Umma. Aidha, Wizara iliendesha  mafunzo ya Mfumo wa Matumizi wa Muda Kati (MTEF) kwa Maofisa 1,089 wakiwemo Wakurungezi wa Sera na Mipango, Makatibu Tawala Wasaidizi wa Mipango, Wakuu wa Idara za  Mipango wa Mamlaka za Serikali za Mitaa na Maofisa wa Bajeti na Mipango kutoka Wizara, Idara zinazojitegemea, Sekretarieti za Mikoa na Mamlaka za Serikali za Mitaa. Kadhalika, Wizara iliendesha mafunzo mbalimbali juu ya uboreshaji wa mifumo ya uandaaji wa bajeti ikiwemo Mfumo wa Uandaaji wa Bajeti kwa kwa kuzingatia Programu (Programme Based Budgeting) pamoja na kuboresha Mfumo wa Takwimu za Fedha za Serikali (GFS) kwa kuzingatia Mwongozo wa Kimataifa wa Takwimu za Fedha za Serikali wa mwaka 2014 (GFSM 2014).

  1. Mheshimiwa Spika, katika kuhakikisha usimamizi wa Bajeti ya Serikali hususan kwenye miradi ya maendeleo, Wizara ilifanya ufuatiliaji wa matumizi ya fedha na kufanya ukaguzi wa miradi mbalimbali ya maendeleo iliyotekelezwa katika kipindi cha mwaka 2014/15 na 2015/16. Aidha, Wizara ilifanya ufuatiliaji wa matumizi ya fedha za Umma katika kipindi cha kufikia mwezi Machi, 2017 katika Halmashauri 73, Baraza la Mitihani la Taifa (NECTA), Ofisi ya Rais – TAMISEMI na matumizi ya fedha za chakula cha wanafunzi wa bweni na fedha za uendeshaji wa shule katika mikoa 11. Vilevile Wizara ilifanya ufuatiliaji wa matumizi ya fedha za kutangaza utalii ndani na nje ya nchi katika Wizara ya Maliasili na Utalii, Bodi ya Utalii Tanzania, Mamlaka ya Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA) na Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro (NCCA). Taarifa zinazotokana na ufuataliaji zinaonesha kuwa bado zipo changamoto zinazotakiwa kufanyiwa kazi katika usimamizi  wa fedha na utekelezaji  wa shughuli zilizopangwa katika maeneo husika.

  1. Mheshimiwa Spika, kazi nyingine zilizotekelezwa katika uandaaji na usimamizi wa utekelezaji wa bajeti ni kama inavyoelezwa katika aya ya 36-37 katika kitabu cha hotuba.

3.4.6 Usimamizi na Udhibiti wa Matumizi ya Fedha za Umma

  1. Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2016/17, Wizara kupitia Idara ya Mkaguzi wa Ndani Mkuu wa Serikali imeendelea kutekeleza majukumu yake ikiwa ni pamoja na kufanya uhakiki wa madeni ya Serikali kwa mwaka wa fedha unaoishia tarehe 30 Juni, 2016 yakiwemo madeni ya walimu hadi kufikia tarehe 31 Desemba, 2015, uhakiki wa wastaafu wanaolipwa pensheni na Wizara na uhakiki wa matokeo ya mradi wa huduma za afya kwenye Mamlaka za Serikali za Mitaa unaofadhiliwa na Mfuko wa Afya na Benki ya Dunia.

  1. Mheshimiwa Spika, majukumu mengine yaliyotekelezwa ni pamoja na kusimamia na kuendeleza Kada ya Ukaguzi wa Ndani na Kamati za Ukaguzi. Katika kutekeleza jukumu hilo, Idara iliendesha mafunzo yanayohusu mbinu za kusimamia vihatarishi katika sekta ya Umma kwa wakaguzi wa ndani 552, wajumbe wa Kamati za Ukaguzi 312, wajumbe wa Kamati za fedha, Uongozi na Mipango 229 kutoka Serikali Kuu na Mamlaka za Serikali za Mitaa, Waratibu wa usimamizi wa vihatarishi 80 na Wajumbe wa menejimenti 75.

3.4.7 Usimamizi wa Malipo   

  1. Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2016/17, Wizara imeendelea kuboresha usimamizi wa malipo kwa kuunganisha mfumo wa malipo wa Tanzania Interbank Settlement System  katika Mamlaka za Serikali za Mitaa 46 zilizopo katika Mikoa ya Dar es salaam, Mwanza, Mbeya, Songwe, Arusha, Dodoma, Tanga na Morogoro. Mfumo wa Malipo wa Electronic Fund Trunsfer umeunganishwa katika malipo ya mishahara ya watumishi waliopo katika Wizara za: Fedha na Mipango; Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto; na Elimu, Sayansi na Teknolojia. Uunganishwaji wa Mifumo hii ya Malipo umeongeza ufanisi katika ulipaji wa malipo ya Serikali na kupunguza gharama za huduma za kibenki. Aidha, Wizara imeendelea kudhamini mafunzo ya muda mrefu kwa watumishi 77 wa kada ya uhasibu, ugavi na kompyuta kutoka kwenye Wizara, Idara za Serikali, Sekretarieti za Mikoa, Mamlaka ya Serikali za Mitaa; na kutoa mafunzo kwa Watumishi wapatao 928 wa kada ya uhasibu kuhusu jinsi ya kutayarisha hesabu kwa kutumia viwango vya kimataifa vya Uhasibu (IPSAS Accrual).

3.4.8 Deni la Taifa

  1. Mheshimiwa Spika, Wizara  imeendelea kusimamia Deni la Taifa kwa kuzingatia Sheria ya Mikopo, Dhamana na Misaada SURA 134. Ili kuhakikisha kuwa Deni la Taifa linahimilika, Serikali inakopa mikopo yenye masharti nafuu ambayo hutumika kwenye miradi ya maendeleo yenye vichocheo vya ukuaji wa uchumi ikiwemo ujenzi wa miundombinu ya barabara, reli, viwanja vya ndege na ujenzi wa mitambo ya kufua Umeme. Aidha, Serikali kwa kushirikiana na wadau kila mwaka na robo mwaka inapitia viwango vya deni la Taifa kila robo mwaka na kwa mwaka mzima ili kuhakikisha kuwa deni linaendelea kuwa himilivu. Vile vile, Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali amefanya ukaguzi wa deni hilo na Serikali inapitia taarifa hiyo na kwamba itazingatia ushauri uliotolewa katika taarifa hiyo.  

  1. Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2016/17, Serikali ilitenga kiasi cha shilingi bilioni 1,218.10 kwa ajili ya kulipa riba ya deni la ndani ambapo hadi kufikia Aprili, 2017 kiasi cha shilingi bilioni 912.87 sawa na asilimia 84 zilitumika. Aidha, Serikali ilitenga shilingi bilioni 617.10 kwa ajili ya kulipia riba ya deni la nje. Hadi Aprili, 2017 shilingi bilioni 456.57 sawa na asilimia 74 zimetumika kulipia deni hilo.

  1. Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2016/17, Serikali ilitarajia kukopa kutoka soko la ndani kiasi cha shilingi bilioni 3,777.11 kwa ajili ya kulipia mtaji (rollover) wa deni la ndani. Hadi kufikia Aprili, 2017 kiasi cha shilingi bilioni 3,963.17 kilikopwa kutoka soko la ndani kwa ajili ya kulipia mtaji wa deni la ndani sawa na asilimia 104.93 ya lengo. Aidha, Serikali ilitenga shilingi bilioni 999.37 kwa ajili ya kulipia mtaji wa deni la nje ambapo hadi kufikia Aprili, 2017 shilingi bilioni 811.0 sawa na asilimia 81 zilitumika kwa ajili hiyo.




3.4.9 Usimamizi wa Mifumo ya Taarifa za Kifedha

  1. Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2016/17, Wizara iliendelea na jukumu lake la uandaaji wa mishahara na usambazaji wa nyaraka za taarifa za mishahara ya watumishi wa umma. Aidha, Wizara inaendelea na kazi ya kuboresha Mfumo wa kutolea taarifa za kulipia mishahara kwa watumishi wa Umma kwa njia ya Kielektroniki (Government Salaries Payment Platform and Government Online Salary Slip Portal) ambao uko kwenye hatua ya usimikaji na utumiaji. Mwezi Aprili, 2017 Wizara tatu ambazo ni Fedha na Mipango; Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto; na Elimu, Sayansi na Teknolojia zimeanza kulipa mishahara kwa kutumia mfumo wa Kielektroniki na kuanzia mwezi Julai, 2017 Wizara, Mikoa, Halmashauri, Taasisi na Wakala za Serikali zilizobaki zitaanza rasmi kutumia mfumo huo.
  1. Mheshimiwa Spika, kwa kutumia Mfumo huu wa Kielektroniki, kila ofisi ya Afisa Masuuli italazimika kuhakiki orodha ya malipo ya mishahara kwa njia ya Kielektroniki kabla ya malipo ya mishahara kufanyika. Orodha ya watumishi waliohakikiwa na kuidhinishwa na Afisa Masuuli ndiyo orodha itakayotumika kwa mwezi husika. Aidha, maboresho haya yatapunguza kwa kiasi kikubwa gharama za uandaaji na usambazaji wa taarifa za mishahara pamoja na kudhibiti mishahara hewa na kufanya Serikali kuokoa kiasi kikubwa cha fedha ambacho kilikuwa kinalipwa kwa watumishi wasio stahili.

3.4.10 Usimamizi wa Mali za Serikali

  1. Mheshimiwa Spika, ili kuhakikisha kunakuwa na usimamizi bora wa Mali za Serikali, Wizara imeendelea kufanya uhakiki wa mali katika Wizara, Idara na Wakala za Serikali ambapo jumla ya hakiki 160 zimefanyika. Aidha, Wizara imefanya uhakiki maalum wa mali za watu binafsi zilizo chini ya uangalizi wa Serikali katika vituo vya Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam. Uhakiki huu ni muhimu kuwa utaipunguzia Serikali mzigo wa kulipa fidia kutokana na mapungufu katika uangalizi na usimamizi wa mali hizo. Vile vile, Wizara imekamilisha uthamini wa ardhi na majengo ya Serikali katika mafungu 16 ili kuwa na taarifa sahihi za mali za Serikali.

  1. Mheshimiwa Spika, Wizara imeendelea na zoezi la uondoshaji wa mali chakavu katika Wizara, Taasisi, Wakala, Mikoa, Idara zinazojitegemea na Mamlaka za Serikali za Mitaa ambapo jumla ya shilingi bilioni 8.42 zilikusanywa kutokana na mauzo ya mali hizo. Aidha, Wizara  imekusanya kiasi cha shilingi milioni 91.71 ikiwa ni fidia kutoka kampuni za Bima kutokana na ajali zilizosababisha uharibifu wa magari ya Serikali na tozo kwa watumishi wa Umma kutokana na upotevu wa mali ya Serikali.

3.4.11 Ununuzi wa Umma

  1. Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2016/17, Wizara imetekeleza yafuatayo: kufanya mapitio ya Kanuni za Ununuzi wa Umma na kukamilisha marekebisho yake ambapo kanuni hizo zimetangazwa kupitia Tangazo la Serikali namba 333 la Desemba, 2016; kutoa mafunzo kwa maafisa 65 wa ununuzi na ugavi Serikalini  juu ya matumizi ya mfumo wa malipo kwa njia ya EPICOR 9; kuboresha Daftari la Maafisa Ununuzi na Ugavi waliopo serikalini na kutoa mafunzo kwa watumiaji 82 wa Daftari hilo; kuandaa Mwongozo wa Utekelezaji wa Shughuli za Ununuzi na Ugavi Serikalini; na kukamilisha zoezi la kufanya tathmini ya ufanisi wa Mfumo wa Ununuzi wa Umma nchini.
  2. Mheshimiwa Spika, shughuli nyingine zilizotekelezwa chini ya  Ununuzi wa Umma, Rufaa za Zabuni za Umma, Huduma ya Ununuzi Serikalini, na Bodi ya Wataalam wa Ununuzi na Ugavi ni kama inavyoelezwa katika kitabu cha hotuba hii kuanzia        uk.31-34.

3.4.12 Ukaguzi wa Hesabu za Serikali

  1. Mheshimiwa Spika,  Ofisi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali ndiyo yenye jukumu la kufanya Ukaguzi wa Hesabu za Serikali. Katika kutimiza jukumu hilo, hadi kufikia  Machi, 2017 ukaguzi wa mwaka 2015/16 umefanyika na ripoti kuu 5 zimeandaliwa na kuwasilishwa kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania tarehe 27 Machi, 2017. Ofisi ilifanya ukaguzi wa hesabu za taasisi za Serikali 199, Wizara na Idara za Serikali zinazojitegemea 54, Mikoa yote 26 ya Tanzania Bara; Wakala wa Serikali 30, Mifuko maalum 13, Mabonde ya Maji 9, Taasisi nyingine za Serikali 25 na Balozi za Tanzania nje ya nchi 34. Aidha, Ofisi ilifanya ukaguzi wa Mamlaka za Serikali za Mitaa 171, Mashirika ya Umma 22 kati ya Mashirika 30 na Vyama vya siasa vitatu (3) kati ya vyama 22.

  1. Mheshimiwa Spika,  Ofisi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) inaendelea na ukaguzi wa miradi ya maendeleo 492 kwenye Halmashauri 171, miradi 40 inayofadhiliwa na Wakala za UNDP, SEDEP II kwa Halmashauri zote zilizopata fedha, TASAF III kwa Halmashauri zote zilizopata fedha za mradi na Global Funds kwa magonjwa ya Malaria, Kifua Kikuu na Ukimwi. Hadi Machi, 2017 ofisi  ilikuwa imekamilisha kaguzi 10 za ufanisi na taarifa kuwasilishwa katika Mamlaka husika. Aidha, Ofisi za Ukaguzi katika mikoa 19 zimeunganishwa na Makao Makuu kwa njia ya mtandao.  Vile vile, Ofisi ya Taifa ya Ukaguzi imeendelea na utekelezaji wa jukumu la ukaguzi katika taasisi 19 za Umoja wa Mataifa kwa mwaka 2016/17.

3.4.13 Usimamizi wa Mashirika na Taasisi za Umma

  1. Mheshimiwa Spika, Wizara kupitia Ofisi ya Msajili wa Hazina ina jukumu la kusimamia rasilimali za Serikali ikiwemo uwekezaji wa Serikali katika Mashirika ya Umma na Kampuni binafsi. Katika kutekeleza jukumu hili, Ofisi ya Msajili wa Hazina husimamia utendaji wa mashirika na taasisi za umma na kutoa ushauri kwa Serikali wa namna ya  kuimarisha uendeshaji wa taasisi, mashirika ya umma na kampuni zipatazo 264. Aidha, Ofisi ya Msajili wa Hazina inasimamia mali ya Serikali ambazo zilibinafsishwa zinazojumuisha viwanda 153 na mashamba 184, lengo likiwa ni kuangalia tija iliyopo na utekelezaji wa mikataba ya mauzo.

  1. Mheshimiwa Spika, katika kutekeleza majukumu tajwa, Ofisi ya Msajili wa Hazina imeendelea na jukumu la kukusanya mapato yasiyo ya kodi. Hadi kufikia Machi, 2017 kiasi cha shilingi bilioni 500.13 zimekusanywa kati ya shilingi bilioni 412.23 zilizopangwa kukusanywa katika kipindi hicho sawa na asilimia 121.32 ya makadirio. Makusanyo hayo yametokana na gawio shilingi bilioni 352.69, michango ya asilimia 15 ya mapato ghafi shilingi bilioni 136.48 na mawasilisho yanayotokana na Mfumo wa Kudhibiti Mawasiliano ya simu za mkononi (Telecommunication Traffic Monitoring System - TTMS) shilingi bilioni 10.96. Aidha, Ofisi ya Msajili wa Hazina imekusanya shilingi bilioni 182.32 kati ya shilingi bilioni 567.45 zilizokadiriwa kukusanywa hadi Machi, 2017 sawa na asilimia 32.13 ya makadirio ya makusanyo kutokana na marejesho ya mtaji uliozidi.

  1. Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2016/17, kampuni zilizotoa gawio kutokana na uwekezaji wa Serikali ni Benki Kuu ya Tanzania (345,787,939,200.00), Inflight Catering Service Limited (223,467,753.77), National Housing Corporation (500,000,000.00), IPS (49,023,840.00), TANICA (4,996,800.00), TCC (670,224,000.00), TLLPPL (53,464,500.00) na TPC (5,399,084,000.00). Aidha, taasisi na kampuni zilizowasilisha asilimia 15 za mapato ghafi katika Mfuko Mkuu wa Serikali ni BRELA (3,716,092,634.00), CMSA (206,785,780.00), DAWASA (2,583,347,512.00), EWURA (5,086,576,093.50), Gaming Board (1,963,466,848.30), Mamlaka ya Hifadhi Ngorongoro (8,750,000,000), Bodi ya Sukari Tanzania (100,000,000), SSRA (805,153,443.15), SUMATRA (3,049,677,255.30), TANAPA (18,844,634,585.82), TANTRADE (32,500,000.00), TBA (331,367,839.16), TBS (4,767,485,399.00), TCAA (5,751,031,516.71), TCRA (12,119,265,150.81), TFDA (1,200,000,000.00), TIRA (1,566,476,454.46), TPA (61,485,500,000.00), TPRI (154,401,054.82), UTT AMIS (92,930,000.00), NACTE (21,889,500.00), NECTA (110,256,443.00), Mzinga (16,432,000.00), OSHA (4,000,000,000.00), Wakala wa Misitu (10,000,000,000.00) na Wakala wa Vipimo na Mizani (1,868,083,157.08).

  1. Mheshimiwa Spika, Ofisi ya Msajili wa Hazina ilifanya ufuatiliaji na tathmini kwenye Taasisi na Mashirika ya Umma 72 yaliyobinafsishwa kwa lengo la kukagua ufanisi na kuhakiki utekelezaji wa masharti ya mikataba ya mauzo.  Matokeo ya ufuatiliji huo pamoja na mambo mengine, yameonesha kwamba wamiliki wa viwanda vinane (8) wamekiuka masharti ya mikataba ya mauzo na kutoonesha nia ya dhati ya kuvifufua. Viwanda hivyo ni:Tembo Chip Board, National Steel Corporation, Mang’ula Mechanical & Machine Tools, Mkata Sawmills, Tanganyika Packers Shinyanga, Kiwanda cha Korosho Newala, Kiwanda cha Korosho Lindi na Mgodi wa Pugu Kaolin. Aidha, hatua mbalimbali za kisheria dhidi ya baadhi ya wamiliki zimechukuliwa ikiwemo kuvirejesha chini ya umiliki wa Serikali. Vile vile, baada ya ufuatiliaji huo Ofisi ya Msajili wa Hazina imechukua hatua mbalimbali kwa mashirika na viwanda vingine vinavyosuasua zikiwemo kuwataka wawekezaji kuongeza uzalishaji.

3.4.14 Mafao ya Wastaafu na Mirathi

  1. Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2016/17, Serikali ilitenga kiasi cha shilingi bilioni 993.61 kwa ajili ya kulipia michango ya mwajiri kwenye Mifuko ya Hifadhi ya Jamii.  Hadi kufikia April, 2017 kiasi cha shilingi bilioni 733.71 sawa na asilimia 73.84 kilitumika kulipia michango ya mwajiri kwa watumishi 540,530  Aidha, Serikali imeendelea kuboresha huduma ya malipo kwa wastaafu ambao wanalipwa na Hazina kwa kulipa pensheni kila mwezi na mirathi moja kwa moja kwenye akaunti zao kwa kutumia mfumo wa TEHAMA wa Benki Kuu ya Tanzania.

  1. Mheshimiwa Spika, Serikali kwa mwaka 2016/17, ilitenga kiasi cha shilingi bilioni 382.62 kwa ajili ya kulipa mafao ya wastaafu na mirathi kwa wastaafu wanaolipwa mafao na Hazina.  Hadi April, 2017 kiasi cha shilingi bilioni 290.89 sawa na asilimia 97.01 kilitumika kulipia mafao ya wastaafu 1,775, mirathi 352 na pensheni kwa kila mwezi kwa wastaafu 55,481.  Aidha, katika juhudi za kurahisisha upatikanaji wa taarifa za wastaafu, kumbukumbu za wastaafu zimeendelea kuhifadhiwa kwenye mfumo wa TEHAMA unaoitwa SAPERION ambapo hadi April, 2017 kumbukumbu za wastaafu 95,092 zilikuwa zimewekwa kwenye mfumo huo.  Kuhusu kima cha chini cha pensheni cha shilingi 100,000 ambacho wastaafu wa PPF walikuwa hawalipwi, kimeanza kulipwa tangu Januari, 2017.

      1. Udhibiti wa Fedha Haramu na Ufadhili wa Ugaidi

  1. Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2016/17, Wizara kupitia Kitengo cha Kudhibiti Fedha Haramu (FIU) imeendelea kusimamia utekelezaji wa Sheria ya Udhibiti wa Fedha Haramu kwa kufanya yafuatayo: kupokea na kuchambua taarifa 208 za miamala shuku inayohusu fedha haramu na ufadhili wa ugaidi; kuwasilisha taarifa fiche za fedha (Financial Intelligence Packages) 37 kwenye vyombo vinavyosimamia utekelezaji wa sheria kwa ajili ya uchunguzi; na kufanya ukaguzi wa taasisi mbili za kifedha. Aidha,  Wizara iliendelea kutoa  elimu kwa wadau jinsi ya kutumia  mfumo maalum wa uchambuzi wa taarifa wa kompyuta (goAML) kwa ajili ya kurahisisha uwasilishaji wa  taarifa za miamala shuku  kwa njia ya kielektroniki na uchambuzi .  Vile vile, kitengo kimekamilisha kanuni za taarifa za usafirishaji na uingizaji wa fedha taslimu kutoka na kwenda nje ya nchi (Cross border declaration of currency reports Regulations) na zimekwishachapishwa. Kadhalika, Kitengo kinaandaa kanuni zitakazozitaka benki kutoa taarifa kwa FIU kila inapofanya miamala ya fedha taslim inayozidi ukomo au kiwango kitakachowekwa.

3.4.16 Tume ya Pamoja ya Fedha

  1. Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2016/17, Wizara kupitia Tume ya Pamoja ya Fedha imekamilisha rasimu ya Stadi ya Uwekezaji katika masuala mbalimbali ya Muungano ambapo jumla ya mashirika tisa (9) yalibainika kuwa yanatekeleza masuala ya Muungano na kwa sehemu kubwa mtaji wake ulitokana na upande mmoja wa Muungano, yaani Tanzania Bara. Mashirika hayo ni:  Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA); Shirika la Ndege Tanzania (ATCL); Benki Kuu ya Tanzania (BOT); Shirika la Maendeleo la Mafuta Tanzania (TPDC); Shirika la Posta Tanzania (TPC); Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL); Benki ya Posta Tanzania (TPB); National Micro Finance Bank (NMB); na National Bank of Commerce (NBC). Vile vile, Tume imekamilisha mapitio ya stadi mbili (2), Stadi ya kubainisha mfumo bora wa kodi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Stadi ya Uchambuzi wa masuala ya fedha yanayohusu mambo ya Muungano. Katika mapitio ya stadi ya mfumo wa kodi, moja ya changamoto zilizofanyiwa kazi ni pamoja na kutambuliwa kwa Kamati za ushauri katika sera za kodi ambayo inajumuisha wajumbe kutoka pande mbili za Muungano kwa kuingizwa katika Sheria ya Bajeti Na. 11 ya mwaka 2015.

      1. Ubia kati ya Serikali na Sekta Binafsi

  1. Mheshimiwa Spika, ushirikishwaji wa sekta binafsi ni muhimu katika kukuza uchumi wa nchi. Hii ni kutokana na ukweli kwamba mahitaji ya miradi ya kiuchumi ni mengi na sekta ya umma pekee haiwezi kufadhili miradi yote. Kwa kuona umuhimu huo, Serikali ilianzisha Kitengo cha Ubia kati ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi ambacho kiko katika Wizara yangu. Kitengo hiki kina kazi ya kuchambua miradi ya ubia iliyowasilishwa na wizara za Kisekta ili kuainisha athari za kibajeti na kuishauri Serikali juu ya utekelezaji wa miradi ya ubia; kutoa mafunzo kwa watekelezaji miradi hiyo na kusimamia masuala ya fedha yanayohusiana na miradi ya ubia.

  1. Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2016/17, Wizara kupitia Kitengo cha Ubia kati ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi, imeendelea kuchambua miradi ya ubia kati ya sekta ya umma na sekta binafsi na kuishauri Serikali juu ya utekelezaji wa miradi hiyo. Miradi iliyofanyiwa uchambuzi katika hatua mbalimbali ni pamoja na: Mradi wa Barabara ya Kulipia ya Dar es Salaam  hadi Chalinze; Mradi wa Mabasi yaendayo Haraka Dar es Salaam Awamu ya pili; Mradi wa Kufua Umeme Megawati 200-350 wa Somanga Fungu Mkuranga; Mradi wa Kufua Umeme wa Kinyerezi III; na Mradi wa Kuzalisha dawa wa Bohari Kuu (MSD).

  1. Mheshimiwa Spika, Watanzania wameanza kupata mafanikio yanayotokana na miradi ya ubia hapa nchini. Kwa mfano Mradi wa  Mabasi Yaendayo Haraka Dar es Salaam umepunguza msongamano wa magari katika  Jiji la Dar es Salaam; muda wa kusafiri kwa mzunguko mmoja umepungua na kwa sababu hiyo huduma  ya usafiri kwenye mradi huo imeongezeka kutoka watu 76,000 kwa siku kwa mwezi Mei, 2016 hadi 180,909 kwa siku kwa mwezi Machi, 2017; Baadhi ya safari kama  vile kutoka Kimara hadi Kivukoni muda wake wakati wa msongamano mkali umepungua kutoka masaa mawili hadi dakika 40; ajira mpya zaidi ya 1,000 zimezalishwa zikihusisha madereva, mafundi karakana, walinzi na wahudumu. Wafanyakazi na wafanyabiashara kwa sasa wanawahi kazini ikilinganishwa na hali ilivyokuwa kabla ya mradi na hivyo kuongeza ufanisi wa kazi; na mandhari ya Jiji la Dar es Salaam imekuwa bora zaidi.

  1. Mheshimiwa Spika, ziko changamoto pia katika miradi ya ubia ikiwa ni pamoja na ukosefu wa wataalam wa kuchambua na kusimamia miradi katika sekta ya umma na sekta binafsi, uelewa mdogo wa jamii kuhusu miradi ya ubia, na ukosefu wa fedha kwa ajili ya kuendeleza miradi ya ubia. Wizara yangu inaendelea kutoa mafunzo kwa sekta husika pamoja na kugharamia baadhi ya vipengele katika upembuzi yakinifu na uendeleaji miradi. Miradi inayogharamiwa katika mwaka 2016/17 ni pamoja na Mradi wa Barabara ya kulipia ya Dar es Salaam hadi Chalinze ( bilioni 1.89), na mradi wa kuzalisha baadhi ya dawa muhimu wa Bohari Kuu ya Dawa ( bilioni 1.0).

3.5 USIMAMIZI NA URATIBU WA TAASISI NA MASHIRIKA YA UMMA CHINI YA WIZARA

  1. Mheshimiwa Spika, Wizara ya Fedha na Mipango inaratibu na kusimamia utendaji kazi wa mashirika na Taasisi za Umma zilizo chini yake. Utekelezaji wa majukumu ya Taasisi na Mashirika haya kwa mwaka 2016/17 ni kama inavyooneshwa katika kitabu cha hotuba kuanzia uk. 44-70.  Aidha, utekelezaji wa miradi ya maendeleo chini ya Wizara kwa mwaka 2016/17, ikijumuisha mafanikio pamoja na changamoto za utekelezaji wa bajeti ni kama inavyoelezwa katika  kitabu cha hotuba uk.70-74.

4.0 MALENGO YA MPANGO NA BAJETI KWA MWAKA 2017/18

  1. Mheshimiwa Spika, baada ya kueleza utekelezaji wa majukumu na bajeti ya Wizara kwa mwaka 2016/17, naomba niwasilishe malengo ya Mpango na Bajeti kwa mwaka 2017/18.

4.1 MAJUKUMU YA WIZARA

4.1.1 Kubuni na Kusimamia Utekelezaji wa Sera za Uchumi Jumla

  1. Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2017/18 Wizara itaendelea kuimarisha Sera za uchumi jumla ikiwemo: kuongeza kasi ya ukuaji wa Pato Halisi la Taifa hadi kufikia asilimia 7.1 mwaka 2017 ikilinganishwa na ukuaji wa asilimia 7.0 mwaka 2016; kuendelea kudhibiti kasi ya mfumuko wa bei na kuhakikisha kuwa unabaki kwenye wigo wa tarakimu moja kufikia asilimia 5.0 Juni 2018; mapato ya kodi kufikia asilimia 14.2  ya Pato la Taifa mwaka 2017/18; kupunguza nakisi ya bajeti (ikijumuisha misaada) kutoka asilimia 4.5 mwaka 2016/17 hadi asilimia 3.8 mwaka 2017/18; na kuwa na akiba ya fedha za kigeni kwa kiwango cha kukidhi mahitaji ya uagizaji wa bidhaa na huduma kutoka nje kwa kipindi kisichopungua miezi minne.

4.1.2 Uratibu wa Mipango ya Maendeleo ya Taifa

  1. Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2017/18, shughuli za kipaumbele zitakazotekelezwa ni pamoja na: kuratibu Utekelezaji wa Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa Miaka Mitano (2016/17-2020/21); kuandaa Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa Mwaka 2018/19; kufuatilia utekelezaji wa Mpango na miradi ya maendeleo; na kuratibu utekelezaji wa Mwongozo wa Usimamizi wa Uwekezaji wa Umma.

4.1.3 Uratibu wa Mikakati ya Kupunguza Umasikini

  1. Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2017/18, maeneo ya kipaumbele ni pamoja na: kukamilisha maandalizi ya Mfumo wa Ufuatiliaji na Tathmini ya Jitihada za kuondoa umasikini yakiwemo Malengo ya Maendeleo Endelevu 2030; kuandaa Taarifa ya Hali ya Umasikini na Malengo Endelevu nchini; kufanya uchambuzi na tathmini ya miradi ya kuondoa umasikini ili kuimarisha jitihada za kuondoa umasikini ngazi ya wilaya na vijiji; kuendelea kuelimisha na kuhamasisha wadau kuhusu  Malengo ya Maendeleo Endelevu na jitihada za kuondoa umasikini; na kuandaa mfumo wa kuibua na kukuza Maendeleo ya Uchumi katika ngazi za chini.

4.1.4 Usimamizi wa Ukusanyaji wa Mapato ya Serikali

  1. Mapato ya Ndani

  1. Mheshimiwa Spika, katika kuboresha ukusanyaji wa mapato ya ndani kwa mwaka 2017/18, Wizara imepanga kutekeleza yafuatayo: kuendelea kusimamia kikamilifu matumizi ya vifaa na mifumo ya kielektroniki ili kuongeza ufanisi na kudhibiti upotevu wa mapato; kuendelea kupanua wigo wa walipa kodi ikiwa ni pamoja na kurasimisha sekta isiyo rasmi ili iweze kuingia katika mfumo wa kodi; kuimarisha ukusanyaji wa mapato yasiyo ya kodi na kuboresha usimamizi wake; kufanya uthamini wa majengo na kusimamia ulipaji ili kuongeza mapato yatokanayo na kodi ya majengo; na kuendelea kuchukua hatua za kudhibiti na kupunguza misamaha ya kodi isiyo na tija.

  1. Misaada na Mikopo

  1. Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2017/18 Washirika wa Maendeleo wameahidi kuendelea kuunga mkono jitihada za Serikali kwa kutekeleza programu na miradi ya kipaumbele iliyoanishiwa katika Mpango wa Maendeleo wa Miaka Mitano (2016/17-2020/21) ambapo wameahidi kuchangia Bajeti ya Serikali kiasi cha shilingi bilioni 3,971.1. Kati ya fedha hizo,  shilingi bilioni 941.2 ni kwa ajili ya Misaada na Mikopo nafuu ya Kibajeti (GBS),  shilingi bilioni 556.1 kwa ajili ya Mifuko ya Pamoja ya Kisekta na shilingi bilioni 2,473.8  kwa ajili ya miradi ya maendeleo.

  1. Mheshimiwa Spika, ili kuimarisha mahusiano na Washirika wa Maendeleo, Serikali imeanza kufanyia kazi mapendekezo ya taarifa ya Washauri Elekezi waliopewa jukumu la kutathmini mfumo mzima wa ushirikiano kati ya Serikali na Washirika wa Maendeleo. Serikali kwa kushirikiana na wadau mbalimbali inaandaa Mwongozo mpya wa ushirikiano unaotarajiwa kutatua changamoto zilizokuwepo hapo awali ambazo zilikuwa zikidhoofisha utekelezaji wa bajeti ya Serikali.

4.1.5 Uandaaji na Usimamizi wa Utekelezaji wa Bajeti ya Serikali

  1. Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2017/18 Wizara imepanga kutekeleza shughuli mbalimbali ikiwemo: kuboresha mifumo ya uandaaji, usimamizi na utekelezaji wa Bajeti ya Serikali; kuendesha mafunzo ya MTEF na Sheria ya Bajeti Na. 11 ya mwaka 2015 kwa wadau mbalimbali; kuandaa machapisho mbalimbali kuhusu Bajeti ya Serikali yakiwemo Mwongozo wa Maandalizi ya Mpango na Bajeti, Makadirio ya Bajeti ya Serikali, Kijitabu cha Bajeti ya Serikali toleo la Wananchi (Citizen Budget) na Taarifa za utekelezaji wa Bajeti ya Serikali; kuandaa na kusimamia utekelezaji wa Bajeti ya Serikali katika Wizara, Idara zinazojitegemea, Sekretarieti za Mikoa na Mamlaka za Serikali za Mitaa; na kufanya tathmini ya utekelezaji wa Bajeti ya Serikali

  1. Mheshimiwa Spika, pamoja na mambo mengine Wizara itaendelea kusimamia na kufuatilia utekelezaji wa bajeti ya mishahara katika Wizara, Idara Zinazojitegemea, Wakala, Taasisi na Mashirika ya Umma, Sekretarieti za Mikoa na Mamlaka za Serikali za Mitaa. Aidha, katika kuimarisha nidhamu ya matumizi ya fedha za umma, Wizara itafanya ufuatiliaji wa mara kwa mara wa matumizi ya fedha za umma kwa Wizara, Idara Zinazojitegemea, Sekretarieti za Mikoa na Mamlaka za Serikali za Mitaa.

4.1.6 Usimamizi na Udhibiti wa Matumizi ya Fedha za Umma

  1. Mheshimiwa Spika, kwa mwaka 2017/18, Wizara itaendelea kufuatilia na kusimamia utendaji wa kada ya ukaguzi wa ndani pamoja na kamati za ukaguzi na kutoa mafunzo kwa kamati za ukaguzi kwa lengo la kuimarisha utendaji kazi wa vitengo vya ukaguzi na kamati za ukaguzi. Aidha, Wizara itafanya ukaguzi wa miradi ya maendeleo, uhakiki wa madeni, uhakiki wa matokeo ya mradi wa huduma za afya kwenye mamlaka za Serikali za Mitaa unaofadhiliwa na Mfuko wa Afya na Benki ya Dunia, ukaguzi maalumu na ufuatiliaji wa utekelezaji wa miongozo ya ukaguzi wa ndani.

4.1.7 Usimamizi wa Malipo
  1. Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2017/18, Wizara imepanga  kuendelea kuunganisha mfumo wa malipo wa TISS katika Mamlaka za Serikali za Mitaa 139 zilizopo katika Mikoa ya Ruvuma, Lindi, Mtwara, Rukwa, Katavi, Tabora, Singida, Manyara, Kilimanjaro, Njombe, Iringa, Pwani, Simiyu, Shinyanga, Mara, Geita, Kigoma na Kagera. Aidha, Wizara imepanga kuendelea kuunganisha mfumo wa malipo wa EFT katika Wizara na Idara zote za Serikali zilizobakia ikiwa ni pamoja na Serikali za Mitaa. Vile vile, Wizara itaendelea kutoa udhamini wa masomo kwa wahasibu, wakaguzi, wagavi na wataalamu wa kompyuta kutoka Serikali Kuu na Serikali za Mitaa waliopo vyuoni.

4.1.8 Deni la Taifa

  1. Mheshimiwa Spika, Wizara kwa mwaka 2017/18, imepanga kuendelea kulipa madeni mbalimbali yaliyokopwa na Serikali ili kugharamia miradi ya maendeleo nchini na kulipa mafao ya wastaafu kwa watumishi wanaolipwa mafao na Hazina mara wanapostaafu na mirathi kwa wategemezi mara mtumishi anapofariki. Aidha, Wizara itaendelea kuwasilisha michango ya mwajiri kwenye Mifuko ya Hifadhi za Jamii ukiwemo Mfuko wa Malipo ya Fidia kwa Wafanyakazi.

4.1.9 Usimamizi wa Mifumo ya Taarifa za Kifedha

  1. Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2017/18, Wizara imepanga kusimika  mfumo wa ukusanyaji  wa taarifa za mapato yasiyokuwa ya kodi; kusimamia kazi ya utengenezaji na uunganishwaji wa mifumo mbalimbali ya kukusanya maduhuli kwenye mfumo mmoja wa Serikali unaoitwa Government Payment Gateway Platform (GePG). Mfumo huu utaanza kutumika katika Taasisi na Idara za Serikali zinazokusanya mapato yasiyo ya kodi. Aidha, Wizara itaendelea kuoanisha na kuunganisha mifumo ya kielektroniki ya kifedha, kusimamia, kuimarisha na kuboresha uendeshaji na utumiaji wa mfumo wa taarifa za mishahara ya watumishi wa umma.




4.1.10 Usimamizi wa Mali ya Serikali

  1. Mheshimiwa Spika, ili kuendelea kutekeleza jukumu lake la kusimamia mali ya Serikali, katika mwaka 2017/18, Wizara imepanga kukamilisha uthamini wa ardhi na majengo ya Serikali kwa Mafungu 36; kuendelea kuondosha mali chakavu, mali sinzia na zilizokwisha muda wake; na kufanya uhakiki maalum wa mali za watu binafsi zilizo chini ya uangalizi wa Serikali na zile zinazotokana na utaifishwaji katika vituo vya polisi nchini. Aidha, Wizara itahakiki mali katika Wizara, Idara zinazojitegemea na Wakala za Serikali ili kutoa ushauri wa kupunguza hasara zinazotokana na matumizi yasiyo ya lazima.

4.1.11 Ununuzi wa Umma

  1. Mheshimiwa Spika, katika Mwaka 2017/18, Wizara imepanga kufanya yafuatayo: kuendelea kutoa mafunzo ya matumizi ya mfumo wa EPICOR 9 katika utekelezaji wa zabuni za umma kwa Maafisa Ununuzi na Ugavi, kutoa mafunzo mbalimbali yanayolenga kuimarisha utekelezaji wa Sheria ya Ununuzi wa Umma Na. 7 ya Mwaka 2011 na kanuni zake za Mwaka 2013 kama ilivyofanyiwa marekebisho Mwaka 2016; na kuandaa na kutekeleza mikakati itakayohusiana na matokeo ya zoezi la Tathmini ya Ufanisi wa Mfumo wa Ununuzi wa Umma nchini.

  1. Mheshimiwa Spika, kazi nyingine zilizopangwa kufanyika ni pamoja na: kusimika na kusimamia mfumo kamili wa ununuzi kwa njia ya mtandao kwenye ununuzi wa dawa, vifaa tiba na bidhaa mtambuka; kufanya ukaguzi kupima uzingatiaji wa sheria ya ununuzi na kupima thamani ya fedha kwa taasisi 120 zilizosajiliwa na Wakala wa Huduma za Ununuzi Serikalini; na kuendelelea kuelimisha wadau mbalimbali kuhusu Sheria ya Ununuzi wa Umma na kanuni zake pamoja na mifumo na nyenzo za utekelezaji wa ununuzi.

  1. Mheshimiwa Spika, Wizara kupitia Wakala wa Huduma wa Ununuzi Serikalini imepanga kuendelea na utaratibu wa ununuzi wa magari ya Serikali kwa pamoja, kuendelea kuandaa mikataba maalumu ya vifaa na huduma mtambuka kwa niaba ya taasisi za Serikali, kuongeza uwezo wa kuhifadhi mafuta katika mikoa ya Kigoma, Lindi, Morogoro na Mtwara, na kuongeza kisima cha kuhifadhi mafuta katika mkoa wa Dodoma.

4.1.12 Ukaguzi wa Hesabu za Serikali

  1. Mheshimiwa Spika,  katika mwaka 2017/18, Ofisi ya Taifa ya Ukaguzi imelenga kuimarisha ukaguzi wa mapato na matumizi ya Serikali na kuhakikisha uwepo wa uwajibikaji na uwazi katika matumizi ya rasilimali za Umma. Ofisi imelenga kufanya yafuatayo: kutekeleza Mpango Mkakati wake wa  Miaka Mitano (2016/17 – 2020/21); kufanya ukaguzi wa mafungu ya bajeti ya Wizara, Idara za Serikali zinazojitegemea, Wakala na Taasisi za Serikali, Sekretarieti za Mikoa, Mamlaka za Serikali za Mitaa, Mashirika ya Umma na miradi ya maendeleo inayofadhiliwa na wahisani. Aidha, Ofisi imepanga kufanya ukaguzi wa kiufanisi na kaguzi maalum katika maeneo yatakayoainishwa, kujenga uwezo wa Wakaguzi katika maeneo mapya ya ukaguzi yakiwemo sekta ya gesi, mafuta na madini, Serikali Mtandao na uhalifu wa kifedha kwa kutumia mtandao na kuboresha mfumo wa ukaguzi kwa kutumia TEHAMA.


4.1.13 Usimamizi wa Mashirika na Taasisi za Umma

  1. Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2017/18, Wizara kupitia Ofisi ya Msajili wa Hazina, itaendelea kufanya ufuatiliaji na tathmini wa Mashirika ya Umma yaliyobinafsishwa. Aidha, Wizara, itaendelea kushirikiana na Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Mifuko ya Jamii, Taasisi za Fedha pamoja na wadau mbalimbali katika suala la uwekezaji na ufufuaji wa viwanda, kampuni na mashamba yaliyobinafsishwa.

  1. Mheshimiwa Spika, Ofisi ya Msajili wa Hazina itaendelea na uhakiki wa mali za taasisi na mashirika ya Umma zilizoingizwa katika Daftari la Mali; kufanya utafiti wa taasisi ambazo zina vyanzo binafsi vya mapato kwa lengo la kuangalia uwezekano wa kupunguza au kuziondoa kwenye utegemezi wa ruzuku ya Serikali; kuongeza mapato yasiyo ya kodi kwa kuimarisha ufuatiliaji wa ukusanyaji kodi kutoka kwa mashirika na taasisi za Umma; kuimarisha usimamizi wa mashirika na taasisi za umma kwa kuingia mikataba ya utendaji; kujenga uwezo wa wajumbe wapya wa Bodi za Wakurugenzi katika usimamizi wa taasisi na mashirika ya Umma; na kuendelea na ukaguzi wa kimenejimenti kwa taasisi na mashirika ya Umma.
4.1.14 Mafao ya Wastaafu na Mirathi

  1. Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2017/18, Wizara itaendelea kuboresha taarifa za wastaafu na kusimamia malipo ya pensheni zinazolipwa moja kwa moja na Hazina.




4.1.15 Udhibiti wa Fedha Haramu na Ufadhili wa Ugaidi

  1. Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2017/18, Wizara itaendelea kusimamia utekelezaji wa Sheria ya Udhibiti wa Fedha Haramu ya Mwaka 2012 na Sheria ya Udhibiti Fedha Haramu na Mali Athirika ya Zanzibar ya Mwaka 2009. Shughuli zifuatazo zitatekelezwa: kuendelea kupokea na kuchambua taarifa za miamala shuku zinazohusu utakasishaji wa fedha haramu na ufadhili wa ugaidi na taarifa za usafirishaji wa fedha kutoka na kuingia nchini kupitia mipakani; kuendelea kuwasilisha taarifa za intelijensia kwenye vyombo vinavyosimamia utekelezaji wa sheria na kukamilisha taarifa ya zoezi la kutathmini mianya na viashiria vya fedha haramu na ufadhili wa ugaidi nchini.

  1. Mheshimiwa Spika, kazi nyingine zilizopangwa ni: kufanya ukaguzi wa watoa taarifa mbalimbali ikiwa ni pamoja na taasisi za fedha; kuandaa na kutekeleza mpango wa mafunzo kwa vyombo vinavyosimamia utekelezaji wa sheria na watoa taarifa wa Tanzania bara na Zanzibar; kuboresha mifumo ya mawasiliano na kompyuta; na kuwajengea uwezo watumishi kujifunza mambo mbalimbali katika nyanja ya udhibiti wa fedha haramu na ufadhili wa ugaidi.

4.1.16 Tume ya Pamoja ya Fedha

  1. Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2017/18, Tume imepanga kukamilisha Stadi ya Uwekezaji katika Mambo ya Muungano, kufanya Mapitio ya Stadi kuhusu Mwongozo wa Uendeshaji wa Akaunti ya Pamoja ya Fedha na kufanya uchambuzi wa takwimu za mapato na matumizi ya Muungano kwa lengo la kuwa na kanzidata ya taarifa za fedha zinazohusu mambo ya Muungano.
4.1.17 Ubia kati ya Serikali na Sekta Binafsi

  1. Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2017/18, Wizara itaendelea kufanya yafuatayo: kupokea na kuchambua miradi ya ubia kwa lengo la kuiidhinisha; kutoa mafunzo ya namna ya kuibua, kuchambua na kutekeleza miradi ya ubia kwenye Wizara, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Taasisi na Mashirika ya Umma na taasisi binafsi; na kuziwezesha Taasisi zenye miradi ya ubia kuajiri washauri elekezi kupitia Mfuko wa Uwekezaji wa Ubia. Aidha, pamoja na kuendelea kutoa elimu kwa wadau mbalimbali kuhusu sera, sheria na kanuni za miradi ya ubia.

4.2    USIMAMIZI NA URATIBU WA TAASISI NA MASHIRIKA YA UMMA CHINI YA WIZARA

  1. Mheshimiwa Spika, mipango na malengo ya bajeti kwa mwaka 2017/18 kwa mashirika na taasisi za umma zilizo chini ya Wizara ni kama inavyooneshwa katika kitabu cha hotuba kuanzia uk.88-103.

  1. MAKADIRIO YA  MAPATO, MATUMIZI  NA MAOMBI YA FEDHA KWA MWAKA 2017/18

    1. MAKADIRIO YA MAPATO

  1. Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2017/18 Wizara inakadiria kukusanya maduhuli kiasi cha shilingi 522,342,627,291 (Bilioni 522.34) kutoka katika vyanzo mbalimbali ikiwa ni pamoja na mauzo ya nyaraka za zabuni, kodi za pango,  mauzo ya leseni za udalali, gawio, marejesho ya mikopo na michango kutoka katika Taasisi na Mashirika ya Umma.

    1. MAOMBI YA FEDHA KWA MWAKA 2017/18

  1. Mheshimiwa Spika, Wizara ya Fedha na Mipango imekadiria kutumia kiasi cha jumla ya shilingi 11,757,125,182,252.00 (Bilioni 11,757.125) kwa mafungu yote tisa.  Kati ya fedha hizo, shilingi 10,328,041,232,511 (Bilioni 10,328.041)  ni kwa ajili ya matumizi ya kawaida na shilingi 1,429,083,949,741.00 (Bilioni 1,429.084) ni kwa ajili ya matumizi ya maendeleo. Matumizi ya Kawaida yanajumuisha shilingi 87,996,020,068.0 (Bilioni 87.996) kwa ajili ya mishahara, shilingi 778,612,212,443.00  (Bilioni 778.612) kwa ajili ya matumizi Mengineyo (OC) na shilingi 9,461,433,000,000.00 (Bilioni 9,461.433) ni Deni la Taifa na Huduma nyingine. Aidha, katika fedha za matumizi ya maendeleo, shilingi 1,382,975,800,000.00 (Bilioni 1,382.976) ni fedha za ndani na shilingi 46,108,149,741.00 (Bilioni 46.108) ni fedha za nje.

MAOMBI YA FEDHA

      1. FUNGU 50 – WIZARA YA FEDHA NA MIPANGO

  1. Mheshimiwa Spika, katika fungu hili kwa mwaka 2017/18, Wizara inaomba kuidhinishiwa kiasi cha fedha kama ifuatavyo:
          1. Matumizi ya kawaida - Shilingi 55,039,643,000.00 (bilioni 55.04). Kati ya fedha hizo:
            1. Mishahara      -    Shilingi 8,077,009,000.00 (bilioni 8.08).
            2. Matumizi Mengineyo – Shilingi 46,962,634,000.00 (bilioni 46.96).
(b)    Miradi ya Maendeleo - Shilingi 11,570,500,000.00  (bilioni 11.57). Kati ya fedha hizo:
  1. Fedha za Ndani - Shilingi 3,500,000,000.00 (bilioni 3.5).
  2. Fedha za Nje   -   Shilingi 8,070,500,000.00 (bilioni 8.07).

      1. FUNGU 21 - HAZINA

  1. Mheshimiwa Spika, katika Fungu hili kwa mwaka 2017/18, Wizara inaomba kuidhinishiwa kiasi cha fedha kama ifuatavyo:
   
  1. Matumizi ya Kawaida – Shilingi 570,429,248,000 (bilioni 570.43)

  1. Kati ya fedha hizo: Mishahara ya fungu hili - Shilingi 40,643,601,000 (bilioni 40.64).
  2. Matumizi Mengineyo – Shilingi 529,785,647,000 (bilioni 529.79) ambazo ni kwa ajili ya matumizi ya idara, taasisi zilizo chini ya Fungu hili, pamoja na matumizi maalum.

  1. Miradi ya Maendeleo – Shilingi 1,395,636,701,741 (Bilioni 1,395.63). Kati ya fedha hizo:

  1. Fedha za Ndani - Shilingi 1,364,000,000,000 (Bilioni 1,364.00).
  2. Fedha za Nje - Shilingi 31,636,701,741 (bilioni 31.63).


      1. FUNGU 22- DENI LA TAIFA

  1. Mheshimiwa Spika, katika fungu hili kwa mwaka 2017/18, Wizara inaomba kuidhinishiwa kiasi cha fedha kama ifuatavyo:
  1. Matumizi ya kawaida – Shilingi 9,472,122,300,000.00 (bilioni 9,472.12). Kati ya fedha hizo:

  1. Mishahara - Shilingi 10,689,300,000.00 (bilioni 10.69).
  2. Matumizi Mengineyo (Malipo ya Madeni na Michango ya Mifuko ya Hifadhi ya Jamii) – Shilingi 9,461,433,000,000.00 (bilioni 9,461.43).

      1. FUNGU 23 – MHASIBU MKUU WA SERIKALI

  1. Mheshimiwa Spika, katika Fungu hili kwa mwaka 2017/18, Wizara inaomba kuidhinishiwa kiasi cha fedha kama ifuatavyo:-
  1. Matumizi ya Kawaida - Shilingi 45,960,838,000.00 (bilioni 45.96).     Kati ya fedha hizo:

  1. Mishahara    –     Shilingi 8,404,104,000.00 (bilioni 8.40).
  2. Matumizi Mengineyo - Shilingi 37,556,734,000.00 (bilioni     37.56).

  1. Miradi ya Maendeleo  – Shilingi 3,600,000,000.00 (bilioni 3.60).     Kati ya fedha hizo:
(i)    Fedha za Ndani - Shilingi 2,000,000,000.00 (bilioni 2.00).
(ii)    Fedha za Nje    -  Shilingi 1,600,000,000.00 (bilioni 1.60).
      1. FUNGU 7 –     OFISI YA MSAJILI WA HAZINA

  1. Mheshimiwa Spika, katika Fungu hili kwa mwaka 2017/18, Wizara inaomba kuidhinishiwa kiasi cha fedha kama ifuatavyo:
(a)    Matumizi ya kawaida – Shilingi 104,917,488,000.00 (bilioni 104.92). Kati ya fedha hizo:-

  1. Mishahara    -           Shilingi       2,687,702,000.00 (bilioni 2.69).
  2. Matumizi Mengineyo -Shilingi 102,229,786,000.00 (bilioni 102.23).

          1. Miradi ya MaendeleoShilingi 2,000,000,000.00 (bilioni 2).     Kati ya fedha hizo:
(i)    Fedha za Ndani – Shilingi 1,000,000,000.00 (bilioni 1).
        (ii)    Fedha za Nje  -Shilingi 1,000,000,000.00 (bilioni 1).

      1. FUNGU 10 – TUME YA PAMOJA YA FEDHA
  1. Mheshimiwa Spika, katika Fungu hili kwa mwaka 2017/18, Wizara inaomba kuidhinishiwa kiasi cha fedha kama ifuatavyo:-
    Matumizi ya Kawaida - Shilingi 1,386,817,511.00 (bilioni 1.39). Kati ya fedha hizo:-
  1. Mishahara - Shilingi 428,676,000.00 (bilioni 0.43).
  2. Matumizi Mengineyo- Shilingi 958,141,511.00
    (bilioni  0.96).




      1. FUNGU 13 – KITENGO CHA KUDHIBITI FEDHA HARAMU

  1. Mheshimiwa Spika, katika Fungu hili kwa mwaka 2017/18, Wizara inaomba kuidhinishiwa kiasi cha fedha kama ifuatavyo:

    Matumizi ya kawaida-Shilingi 1,515,586,000.00 (bilioni 1.52).

      1. FUNGU 45 – OFISI YA TAIFA YA UKAGUZI

  1. Mheshimiwa Spika, katika Fungu hili kwa mwaka 2017/18, Wizara inaomba kuidhinishiwa kiasi cha fedha kama ifuatavyo:

  1. Matumizi ya kawaida – Shilingi 61,832,948,000.00 (bilioni 61.83). Kati ya fedha hizo:
  1. Mishahara - Shilingi 17,313,756,000.00 (bilioni 17.31).
  2. Matumizi Mengineyo - Shilingi 44,519,192,000.00 (bilioni 44.52).

  1. Miradi ya Maendeleo – Shilingi 11,800,948,000.00 (bilioni 11.80).  Kati ya fedha hizo:
(i)    Fedha za Ndani – Shilingi 8,000,000,000.00 (bilioni 8.00).
(ii)    Fedha za Nje          -     Shilingi 3,800,948,000.00
    (bilioni 3.80).

      1. FUNGU 66 – TUME YA MIPANGO

  1. Mheshimiwa Spika, katika Fungu hili kwa mwaka 2017/18, Wizara inaomba kuidhinishiwa kiasi cha fedha kama ifuatavyo:-

  1. Matumizi ya Kawaida  - Shilingi 4,936,364,000.00 (bilioni 4.93).  Kati ya fedha hizo:
  1. Mishahara    –    Shilingi  1,603,212,000.00 (bilioni 1.60).
  2. Matumizi Mengineyo – Shilingi 3,333,152,000.00 (bilioni  3.33).
  1. Miradi ya Maendeleo   – Shilingi 4,475,800,000.00  (bilioni 4.47)     ambazo ni fedha za Ndani.
   
    1. SHUKRANI

  1. Mheshimiwa Spika, naomba nitumie fursa hii kuzishukuru nchi na mashirika mbalimbali ya kimataifa ambayo kwa namna moja ama nyingine yamesaidia katika utekelezaji wa bajeti ya Wizara. Aidha, napenda kuwashukuru sana Wafanyakazi na wananchi wote ambao wameendelea kulipa kodi kwa hiari na pia kushiriki katika ujenzi wa Taifa letu.

  1. Mheshimiwa Spika, mwisho kabisa napenda kuwashukuru Waheshimiwa Wabunge wote kwa kunisikiliza. Hotuba hii inapatikana katika tovuti ya Wizara (www.mof.go.tz).

  1. Mheshimiwa Spika, naomba kutoa hoja.






Post a Comment

karibu kwa maoni

 
Top