0
Benny Mwaipaja, WFM-Dodoma

Wizara ya Fedha na Mipango imeliomba Bunge iidhinishie makadirio ya mapato na matumizi (Bajeti) ya zaidi ya shilingi trilioni 11.757 ili iweze kutekeleza majukumu yake kwa mwaka wa fedha 2017/2018, kwa mafungu yote 9 yaliyochini ya Wizara hiyo.

Maombi hayo yametolewa na Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Mpango, wakati akiwasilisha makadirio ya mapato na matumizi ya Wizaya hiyo, Bungeni Mjini Dodoma, leo.

Dkt. Mpango amesema kuwa kati ya fedha hizo, shilingi trilioni 10.328  ni kwa ajili ya matumizi ya kawaida na shilingi trilioni 1.429 ni kwa ajili ya matumizi ya maendeleo.

Amefafanua kuwa Matumizi ya Kawaida yanajumuisha shilingi bilioni 87.996 kwa ajili ya mishahara, shilingi bilioni 778.612 kwa ajili ya matumizi Mengineyo (OC) na shilingi trilioni 9.461 ni kwa ajili ya kulipa Deni la Taifa na Huduma nyingine.

Aidha, katika fedha za matumizi ya maendeleo, shilingi trilioni 1.382 ni fedha za ndani na shilingi bilioni 46.108 ni fedha za nje.

Post a Comment

karibu kwa maoni

 
Top