TIMU
ya Kagera Sugar ya Bukoba imesajili wachezaji sita wapya, akiwemo beki
wa zamani wa kimataifa wa Tanzania na klabu ya Simba, Juma Said Nyosso.
Nyosso anasajiliwa Kagera Sugar baada ya kumaliza adhabu yake ya kufungiwa miaka miwili kufuatia kumtomasa makalio mshambuliaji John Raphael Bocco akiwa Azam FC kabla ya kuhamia Simba wiki hii.
Mbali na Nyosso ambaye alifungiwa akiwa anachezea Mbeya City mwaka juzi, Kagera Sugar pia imemsajili kipa Hussein Kipao kutoka JKT Ruvu iliyoshuka Daraja kutoka Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara msimu

Wengine
ni beki Japhary Kibaya kutoka Mtibwa Sugar ya Morogoro, viungo Peter
Samson Mwalyanzi, Ludovic Venance na mshambuliaji Omary Daga maarufu
‘Dagashenko’ wote kutoka Africa Lyon iliyoshuka Daraja pia.
Tayari Kagera Sugar imempoteza mshambuliaji wake tegemeo, Mbaraka Yussuf Abeid aliyesaini Azam FC wiki iliyopita, huku pia kiungo Babu Ally Seif akiripotiwa kuwa mbioni kujiunga na Yanga.

Post a Comment
karibu kwa maoni