Takribani
watu tisa wamejeruhiwa na majambazi baada ya kundi la watu
wanaosadikiwa kuwa majambazi kuvamia mgodi wa dhahabu uliyopo katika
kijiji cha Nyakivangala, Isimani wilayani Iringa mkoani Iringa.
Mbali
na kujeruhi, majambazi hao wamepora zaidi ya Shilingi Milioni 81,
dhahabu zaidi ya gramu 400, na baadhi ya mali za wafanyabiashara katika
eneo hilo.
Akizungumzia
tukio hilo, Mkuu wa wilaya ya Iringa ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati
ya Ulinzi na Usalama katika wilaya hiyo, Richard Kasesela amesema tukio
hilo lililitokea majira ya saa nne usiku.
Kasesela
amesema kuwa Jeshi la Polisi linasaka majambazi hao huku akieleza kuwa
Serikali inashirikiana na wananchi wa eneo hilo kuhakikisha kituo cha
Polisi kinajengwa ili kuimarisha usalama wa wananchi katika maeneo hayo.
Aidha,
amewataka watu wanaofanya shughuli zao katika maeneo hayo kuchukua
tahadhari ikiwa ni pamoja na kutokutembea na kiasi kikubwa cha fedha
kwani sasa teknolojia imekuwa hivyo wanaweza kuhifadhi pesa zao hata
kupitia mitandao ya simu.
Post a Comment
karibu kwa maoni