0


Responsive imageMkuu wa mkoa wa Manyara Dakta Joel Bendera ameiagiza Halmashauri ya wilaya ya Kiteto kufanya marekebisho ya meza na viti 300 vilivyotengenezwa chini ya kiwango kwa ajili ya Shule za sekondari wilayani humo.
 Dkt. Bendera amebaini kasoro hizo baada ya kukagua Samani za shule ya Sekondari Engusero na Kiteto zilizoandaliwa kwa ajili ya wanafunzi wanaotarajiwa kuanza kidato cha tano katika shule hizo mwaka huu.
 Kutokana na kasori hizo Dkt.Bendera  amemtaka Mkuu wa Chuo cha ufundi cha VETA mkoa wa Manyara kutoa maelezo kuhusiana na tatizo hilo kwakuwa chuo ndicho kilichohusika na matengenezo ya samani hizo.

Post a Comment

karibu kwa maoni

 
Top