0
Mtafiti Mkuu na Mkurugenzi wa Teknolojia ya Habari na Mawasiliano kutoka Taasisi ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu, Leonard Mboera akiwasilisha mada.
TAASISI ya Utafi ti wa Magonjwa ya Binadamu (NIMR) imetoa matokeo ya utafi ti wa vifo vinavyotokea katika hospitali za Tanzania katika kipindi cha miaka 10 kuanzia mwaka 2006 hadi 2015 na kuonesha kuwa vifo vya watoto chini ya miaka mitano, vilichangia asilimia 20 ya vifo vyote 247,976 vilivyotolewa taarifa katika kipindi hicho.
Mtafiti Mkuu Kiongozi wa taasisi hiyo, Dk Leonard Mboera alisema hayo jana kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi, Mkuu wa Wilaya ya Morogoro, Regina Chonjo kufungua warsha ya siku mbili ya watafiti wa magonjwa ya binadamu kutoka taasisi hiyo kuhusu sababu za vifo katika hospitali nchini.
Alisema matokeo ya utafiti huo yameonesha vifo vingi viliathiri kundi la watu wenye umri wa miaka 30-45 ambapo wengi hufa wakiwa na wastani wa umri wa miaka 31 ama kufikia miaka 33 kwa wanaume na wanawake ni miaka 29.
Katika kipindi cha utafiti huo, jumla ya vifo 247,976 viliripotiwa ambako kulikuwa na tofauti kubwa kati ya idadi ya vifo, kati ya jinsia ya kiume na ya kike na kwamba vifo vingi viliathiri zaidi wanaume kuliko wanawake.
Kwa mujibu wa Dk Mboera, utafiti huo uliofanyika kati ya Julai na Desemba 2016 na kuhusisha hospitali kadhaa ikiwamo Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, Hospitali za Rufaa za Kanda na mikoa, hospitali maalumu na hospitali za wilaya kubaini maradhi yanayowaathiri zaidi Watanzania, vifo vingi vilitokea katika hospitali za mikoa ya Dar es Salaam, Morogoro na Mwanza ambako vifo katika kundi la watoto nchini ya miaka mitano vilichangia asilimia 20 ya vifo vyote.
Alitaja magonjwa yaliyoongoza kusababisha vifo ni malaria iliyosababisha vifo vya watu 28,219 sawa na asilimia 12.75, magonjwa ya mfumo wa hewa kwa vifo vya watu 22,316 sawa na asilimia 10.8 na Ukimwi kwa watu 17,790 sawa na asilimia 8.0.

Post a Comment

karibu kwa maoni

 
Top