Mapacha walioungana kuanzia kifuani hadi tumboni wamefariki dunia jana
katika hospitali ya Taifa Muhimbili jijini Dar es Salaam walipokuwa
wakipatiwa matibabu baada ya kuzaliwa katika hospitali ya Berege
wilayani Kilosa mkoani Morogoro.
Afisa
uhusiano wa hospitali ya Taifa Muhimbili, Neema Mwangomo amethibitisha
kufariki kwa watoto hao ambao walikuwa wakisubiri kufanyiwa upasuaji,
huku akisema kuwa uchunguzi unafanyika kubaini chanzo cha kifo cha
watoto hao.
Watoto hao waliozaliwa wakiwa na uzito
wa kilo nne walipewa rufaa ya kupelekwa katika Hospitali ya Taifa
Muhimbili ili kupatiwa uangalizi zaidi na waliwasili katika hospitali
hiyo Juni 24 na kuwekwa katika chumba cha uangalizi maalum.
Daktari bingwa wa upasuaji wa watoto,
Dkt. Zaituni Buhari Agosti 2 mwaka huu alieleza wanahabari kuwa watoto
hao walikuwa wanachangia ini na sehemu ndogo ya moyo lakini wangeweza
kufanyiwa upasuaji.
Hata hivyo baadhi ya mapacha wa aina
hiyo ambao hawajawahi kufanyiwa upasuaji na kufanikiwa kuishi na kuwa
watu wazima ni pamoja wale wanaoishi wilayani Kilolo mkoani Iringa na
wamehitimu kidato cha sita mwaka huu na kupata ufaulu mzuri wa kuendelea
na elimu ya juu..
Post a Comment
karibu kwa maoni