Madereva pikipiki 'bodaboda' wametakiwa kuwa mstari wa mbele katika
kufichua vijana wanaojishughulisha na shughuli za uhalifu kwa kutumia
kivuli cha bodaboda ili kuondokana na na vitendo vya uhalifu.
Akizungumza
na madereva wa pikipiki wa kijiji cha Kwa Mtoro wilayani Kondoa mkoani
Dodoma wakati akifunga mafunzo ya usalama barabarani, Mkaguzi Msaidizi
wa polisi Jackson Sizya amesema bodaboda wengi wamekuwa wakitumika
vibaya katika kuchochea vitendo vya kiuhalifu hivyo ni muda sahihi kwa
wao kujiweka mbali na matukio hayo.
"Mmekuwa mnatumiwa na
wahalifu kwa sababu ni wepesi wa kukwepa ni vyema mkawa mabalozi wazuri
wa vyombo vya dola kuwafichua wahalifu na siyo kushirikiana nao na
kuwapeleka mafichoni. Hatutegemei nyinyi mlioshiriki mafunzo haya
mkawabeba wahalifu kwenda hata kuvamia benki. Kwa sheria za Tanzania
mtawachukuliwa wote adhabu sawa" alisema
Katika hatua nyingine mkaguzi huyo
amewataka madereva wa pikipiki maarufu bodaboda kutumia vyema elimu ya
usalama barabarani katika kuondokana na ajali za barabarani
"Ni matumaini yangu kwamba
mtaenda kupunguza ajali, kuokoa maisha ya watu wengine, na kusimamia
usalama barabarani. Nendeni mkarejeshe amani kwa abiria wenu kwa kuanza
safari salama na kumaliza salama siyo kutengeneza huzuni," aliongeza.
Post a Comment
karibu kwa maoni