Halmashauri ya Manispaa ya Ilala Jijini Dar es Salaam imeanza zoezi la
kuzifungia Shule binafsi za msingi na za awali zipatazo 125 kwa
kuendeshwa kinyume cha sheria ikiwemo kukosa usajili na kutokuwa na eneo
la kutosha kuendeshea shule hizo.
Afisa
Elimu wa shule za msingi katika manispaa ya Ilala jijini Dar es Salaam,
Bi. Elizabeth Thomas amesema kuwa, mpaka sasa wamezifungia shule zaidi
ya 25 huku wakibaini mapungufu mengi ikiwa ni pamoja na baadhi ya shule
kubandika namba ya usajili feki wakati haikusajiliwa, kukosa vyoo na
vingine zikijiendesha kinyume cha utaratibu.
Akitaja Baadhi ya shule zilizokwisha kufungwa kuwa ni pamoja na Mbingaa Nursery & Primary school English Medium, Montessori Nursery School & Proficience College Ilala, Morning Star,Gift Academy, New Generation na nyingine nyingi
Aidha Afisa huyo amewataka wazazi kujenga tabia ya kufuatilia usajili wa shule kabla ya kuwandisha watoto ao ilikuepuka usumbufu unaojitokeza baada ya shule hizo kufungiwa

Post a Comment
karibu kwa maoni