Na Gharos Riwa—BUNDA 0768 44 33 15
BUNDA
Mkuu wa wilaya ya Bunda Mwalimu
Lydia Bupilipili amewataka wakazi wa wilaya hiyo kuwa tayari kwa mapokezi ya
mbio za mwenge wa uhuru unaotarajiwa kuwasili hivi karibuni.
Amesema hayo wakati akiongoza
wananchi wa halmashauri ya mji wa bunda katika kutimiza agizo la Makamu wa Rais
Samia suluhu Hasani ya wananchi wote kushiririki michezo kila jumamosi ya pili
ya kila mwezi, ambapo amesaema kuwa mwenge huo wa uhuru unatarajiwa kufika
wilayani hapa tarehe 23 Agost 2017
ambapo utazindua na kutembelea miradi mbalimbali iliyotekelezwa na serikali.
Bupilipili amesema wataupokea mwenge
huo wa uhuru kisorya, na utapita kuangalia miradi ya serikali ikiwemo zahanati
ya Nansimo,shule ya sekondari nansimo, kasahunga,bulamba na baadae Makongoro
sekondari na hatimae mwenge huo utalala Nyamuswa.
Aidha Mkuu huyo wa wilaya amesema
kuwa baada ya mwenge huo kulala
nyamuswa, tarehe 24.8. 2017
mwenge huo wa uhuru utaingia halmashauri ya mji wa bunda na utapokelewa
kisangwa ambapo baadae utaendelea kukimbizwa katika hospitali ya Manyamanyama
na katika kikundi cha maji cha Stop Over , pia utatembelea kiwanda cha
kutengeneza mikate Bunda Bekary na hatimae shule ya sekondari ya wasichana
ya ACT ya kanisa la Angilikana, ambapo baada ya kutembelea miradi hiyo
utalala mjini hapa katika eneo la standi mpya.
Hata hivyo ametoa wito kwa wakazi
wote wa wilaya ya bunda kujitokeza kwa wingi katika mapokezi ya mwenge huo kwa
kuwa mwenge wa uhuru una hadhi ya Rais wa Nchi.
Post a Comment
karibu kwa maoni