|
Rais Magufuli amefunguka na kusema kuwa Tanzania inahitaji sana
wawekezaji kuja kuwekeza nchini lakini wawekezaji ambao wanajifanya kuja
kuwekeza kwa kigezo cha kuiba mali za nchi na Watanzania hao hawatakiwi
na bora wasije kabisa nchini.
Rais Dkt. John Pombe Magufuli akihutubia wananchi wa Mererani wakati
wa kuzindua barabara ya lami ya kilomita 26 kutoka Uwanja wa Ndege wa
kimataifa wa kilimanjaro (KIA) mkoa wa Kilimanjaro hadi Mererani Manyara
Septemba 20, 2017.
Magufuli
amesema hayo leo Septemba 20, 2017 akiwa Mkoani Manyara wilaya ya
Simanjiro katika ziara yake ya kikazi wakati akizindua barabara na
kusema wawekezaji ambao wanataka kuja kuwekeza ili kuiba maliasili za
nchi ni bora wasije kwani hawatafanikiwa chini ya utawala wake wa awamu
ya tano.
"Tanzania tunahitaji
wawekezaji lakini si wawekezaji wanaotaka kutuibia, kama unataka kuja
kuwekeza Tanzania kwa kisingizio cha kuja kutuibia ni bora usije, kwani
utakuwa umeula wa chuya kwa sababu wakati huu hautaiba, nasema huyo
mwekezaji atalia na hili nalisema kwa uwazi kwa sababu tumeamua
kupambana kwa ajili ya vita ya uchumi kwa ajili ya taifa letu" alisema Rais Magufuli
Rais Magufuli aliendelea kusisitiza kuwa mataifa makubwa na
wawekezaji kutoka nje wametujengea mawazo kuwa wao ndiyo wenye mali na
uwezo kumbe wao hawana hizo mali na uwezo bali sisi ndiyo wenye mali na
uwezo huo kuliko wao ambao wanategemea maliasili zetu.
"Tanzania ni tajiri mno,
wametujengea 'element' kwamba sisi hatuna wao wanacho, kumbe sisi ndiyo
tunacho wao hawana, wengine wanajifanya wafadhili, ndugu zangu viongozi
tusimamie rasilimali za nchi yetu nafahamu katika hatua ambazo tumeanza
kuchukua wapo baadhi ya watu wameanza kukimbia, wengine hamtawaona
wamekimbia kwa sababu wameona walichokuwa wanakifanya ni cha hovyo" alisisitiza Rais Magufuli |
|
|
Rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwapungia mkono maelfu ya wananchi katika kijiji cha Nyaisinyai Mererani Manyara. |
|
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt John Pombe Magufuli
amezindua barabara ya Kilometa 26 ya KIA -Mererani Mkoa wa Manyara leo.
Rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli
akilakiwa kwa furaha na Mkuu wa Mkoa wa Manyara Mhe. Dk.Joel Bendera
alipowasili kuzindua barabara ya lami ya kilomita 26 kutoka Uwanja wa
Ndege wa kimataifa wa kilimanjaro (KIA) katika mkoa wa Kilimanjaro hadi
Mererani mkoani Manyara Septemba 20, 2017. | | | | | | | | | | | | | | |
Post a Comment
karibu kwa maoni