0
KIUNGO Mnyarwanda, Haruna Hakizimana Fadhil Niyonzima hatakuwepo kwenye kikosi cha Simba Jumapili katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara dhidi ya Mwadui FC ya Shinyanga kutokana na kuwa majeruhi.
Taarifa hiyo aliitoa Kocha Msaidizi wa Simba, Mganda Jackson Mayanja na kueleza kwamba Haruna aliumia mazoezini wiki hii na hataweza kucheza katika mchezo wa leo.
Pamoja na Haruna, Mayanja amesema beki wa kulia, Shomari Kapombe ataendelea kukosekana, wakati mshambuliaji Juma Luizio naye ameingia kwenye orodha ya majeruhi na hatakuwepo.
Simba SC iliuanza msimu huu wa Ligi Kuu vizuri, ikishinda mabao 7-0 dhidi ya Ruvu Shooting Agosti 26 Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam kabla ya kwenda kulazimishwa sare ya 0-0 na Azam FC Uwanja wa Azam Complex, Chamazi Septemba 9.

Post a Comment

karibu kwa maoni

 
Top