0
Gari la polisi lililokuwa limebeba mahabusu jana lilipata ajali eneo la
kenyata jijini mwanza kwenye mzunguko wa samaki na kusababisha mahabusu
mmoja na askari kupata majeraha.



Gari
hilo lenye namba za usajili PT 3643 aina toyota land cruiser pick up
lililokuwa limetoka mahakama ya wilaya ya Nyamagana likuwa limewabeba
mahabusu wanaodaiwa kuwa ni hatari waliokuwa wanarudishwa gereza la
butimba na ghafla lilipofika eneo la mzunguko wa samaki gari namba T 230
BMP aina ya toyota vitz lililookuwa linaendeshwa na happyness clorence
ambapo aliliweza kuingia ghafla barabarani na kupelekea ajali hiyo
kutokea.
kamanda wa jeshi la polisi mkoani mwanza
naibu kamishna ahmed msangi amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo na
kusema majeruhi wamepatiwa matibabu katika Hospitali ya rufaa ya mkoa wa
mwanza Sekou Toure na kuweza kuruhusiwa.
"Madereva wengi wana dharau
na ndiyo maana ajali kama hizi huwa zinatokea. kwa hili lilotokea
lingeweza kusababisha matatizo makubwa mno kwani askari wetu walikuwa
wapo na silaha nzito na mahabusu waliokuwa wakisindikizwa walikuwa
hatari kwani wangeweza kuumia au kupata fursa za kukimbia na ukizingatia
askari walikuwa na silaha yangetokea mengine makubwa"
Ahmed Msangi.

Post a Comment

karibu kwa maoni

 
Top