Akizungumza katika mkutano na wakazi wa vijiji vya Gendabi,Sebasi,Hargushay na
Sarjanda vyote vikiwa vinaunda kata ya
Gendabi Kamishina msaidizi wa wizara ya
nishati na madini kanda ya kasikazini
Bw.Adam Juma alieleza kuwa mgogoro huo ulitokana na fedha zilizokuwa zikitolewa na serikali kwa ajili ya kusaidia vikundi vidogo vidogo
vya wachimbaji wa madini kwa ajili
ya kuwakwamua na kuwapa ari ya kufanya kazi.
Jumla ya
vikundi 59 vilivyosajiliwa
nchini hapa vimenufaika na fedha hizo za
serikali huku mkoa Wa manyara ukijwa kuwa na vikundi 6 ambapo kukindi
kimojawapo ni cha uchimbaji wa chumvi katika mgondi wa chumvi wa Hargushay kinachofahamika kwa majina ya
Hasami kinachochimba chmvi katika mgondi
huo pamoja na kuuza.
Mgodi wa Hargushay unaelezwa kuwa na vikundi
viwili ambavyo ni Gesami na Hasami
lakini ikaelezwa kuwa kikundi
kilichosajiliwa ni hasami na ndicho
kinatakiwa kupata fedha hizo jumla ya
million 90 ambapo kwa pande mwingine kulitokea kutoelewana kati ya vikundi
hivyo huku wote wakidai wapo kihalali bila kujali kama hwajasajiliwa.
Naye mkuu wa wilaya ya Hanang’ Sarah Msafiri alieleza chumvi inazalishwa katika mgondi huo
imekuwa ikisafirishwa kwenda nchi za Rwanda,Burundi,Kenya na Malawi
kwa ajili ya matumizi mabalimbali lakini mafanikio ni kdogo ikilinganishwa na uchimbaji
unaofanywa katika mgondi huo na hiyo ni kutokana na kukosa usimamizi wa kukusanya mapato katika njia
zilizosahihi hivyo kuisababishia hasara halmashauri na hata wao wenyewe kutokana
na kufanya uuzaji holela.
‘’Ndugu
zangu tumekuja hapa leo ili tumalize
mgogoro uliokuwa ukiendelea hapa na kusababisha
magari yanayosafirisha na kununua chumvi kusimamishwa kwa madai kuwa
hawaruhusiwi kusafirisha mpaka wapate kibali cha mamlaka ya hali ya hewa [TMA]
ndipo waweze kusafirisha lakini leo tumemaliza suala hilo na Kamshina wetu na sasa wasafirishaji na
wanunuzi watafanya kazi hiyo kama ilivyokuwa siku zote’’alisema Bi. Sarah.
Awali kabla
ya mgodi huo kuwa chini ya halmashauri ulielezwa kukusanya kwa mwaka jumla
ya Million 19 kwa mwaka ambazo
wanakikundi walikuwa wakigawana lakini
badala ya Halmashauri hiyo kugundua inakosa
mapato makubwa katika Mgondi huo
waliamaua kupeleka mashine za EFD’s kwa ajili ya ukusanyaji Ushuru wa mapato yanayotokana na uuzaji wa chumvi hiyo na walifanikiwa kukusanya jumla ya Million 117 kwa mwaka.
‘’ Kwa kuwa tumekubaliana na kamishna kwa sasa
tutaendelea kutumia mashine hizi ambapo makato yatakuwa ya moja kwa moja ya ushuru kwenye mashine ile kutakuwa na ushuru
wa Wizara ya madini
ambao utakuwa unakatwa moja kwa moja na
sisi halmashauri tutakata fedha
yetu ya ushuru haya ndio makubaliano yetu na nafikiri kama tu tumefanya usimamizi mzuri na
tukakusanya million 117 na ukiangalia
ukubwa wa mgondi wetu unaturuhusu kupata fedha zaidi ya hiyo ila usimamizi ndio haukuwa sawa ila kwa sasa
tayari tumemuweka mkusanya ushuru
ili tusipoteze tena mapato ‘’ alisema Bi. Sarah.
Madini hayo
aina ya chumvi katika mgodi wa Hargushay
yameelezwa kupatikana kwa msimu ambapo inakuwa ni kiangazi na wakati wa kipindi
cha masika maji hujaa ivyo huwalazima kusubiri maji yakauke ndio waweze kuvuna chumvi lakini mkuu wa wilaya
akawahakikishia endapo kutakuwa na usimamizi bora utaohusisha wataalamu chumvi
hiyo itavunwa muda wote na syo kwa msimu.
Naye mkurugenzi mtendaji wa wilaya ya Hanang’ Bryceson Kibassa alieleza mradi huo haujatumiwa vizuri ili kuwanufaisha
wananchi wa vijiji hiyo na kubadili maisha yao
kutokana na mgondi ho kuwa na
mgogoro kati yao wanavjiji k na chumvi kuzalishwa kwa kiasi kikubwa na kuuzwa kwa bei ya chini
ambapo kwa sasa ngunia linauzwa kwa Tsh 1000.
Aidha alieleza kuwa kinachotakiwa ni kuendelea
kuweka kiwango cha juu kcha uuzaji wa
chumvi paoja kuboresha bora wa chumvi hiyo ili kuweza kupata masoko ya uhakika na yatakayowanuisha wazalishaji wa chumvi.
Ayubu
Ramadhani ni msafirishaji wa chumvi ni mmoja kati ya
wasafirishaji ambao magari yao yalisitishwa kusafirisha chumvi kutoka mgodi wa
Hargushay ambaye anapeleka chumvi hiyo
Nairobi alieleza kuwa ni miaka miwili
sasa toka ajiingize kwenye biashara ya
chumvi lakini hali bado
haijabadilika licha ya wao kutoa ushuru halmashaur kwani miundo mbinu ya barabara
hiyo ina makorogo haina
galavati hivyo imekosa hadhi ya kusafishia magari ya mizingo mikubwa na mizito hivyo
waliomba serikali kuwaboreshea
barabara ili waweze kusafirisha
kiurahisi.
Chumvi ya
Gendabi inaelezwa kuuzwa nchi za nje
kwa ajili ya kukaushia ngozi, kubadilishana chumvi na mahindi au vitu
vingne na nyingine hutumika kwa matumizi ya kawaida ya kupikia.
Wakazi wa
kata hiyo waliomba kuboreshewa soko la
chumvi hiyo ambayo imeonekana kushuka kwa kiasi kikubwa kutoka elf tatu waliyokuwa wakiuza kwa mwaka jana mpaka kufikia elfu 1000 ambayo imekuwa ni kidogo
na kushindwa kuwasaidia kwa kiasi kikubwa kwani wengi hutengemea kuuza chumvi
kwa ajili ya kupata fedha ya matumizi pamoja na kuwasomeshea watoto wao.
Aidha
mkuu wa wilaya amewataka wananchi
wa vijiji hivyo kuendelea kujiunga na vikundi ikiwa ni pamoja na kuanzisha
vikundi vipya na kuvisajili ili viweze kupata leseni na kunufaika na fedha za seikali huku
akieleza kuwa lengo ni kufikia vikundi 100 vya ujimbaji chumvi katika mgodi
huo.
Post a Comment
karibu kwa maoni