0
na gharos riwa -bunda

Siku chache baada ya mtandao huu  kuripoti habari kuhusu mifugo zaidi ya 700 kufa kwa tatizo la kukosa maji na majani kwa muda mrefu, hatimae leo mkuu wa idara ya mifugo na uvuvi wa halmashauri ya mji wa bunda Mkoani Mara bwana Rick steven Kaduri amejitokeza na kupinga ukweli wa taarifa hiyo licha ya kukiri kuwa mifugo imekufa.

Amesema kuwa ni kweli mifugo imekufa katika halmashauri ya mji wa bunda, lakini ameshangazwa na idadi iliyotajwa ya mifugo zaidi ya  700 kufa huku akisema kuwa kwa taarifa walizonazo kama halmashauri nzima ni zaidi ya mifugo 1000 imekufa kwa kukoswa maji na majani kwa muda mrefu.

Amesema taarifa kama hizo zilisikika tena guta kuwa zaidi ya ng’ombe 3000 wamekufa lakini bado wanazidi kuzifanyia uchunguzi kubaini ukweli wake.



Amesema tatizo la mifugo kufa imetokana na ukame wa muda mrefu huku akitaja kuwa wafugaji waliokuwa na ng’ombe wenge ndio waathirika wakubwa hivyo amewakumbusha wafugaji kufuga kisasa ili waweza kumudu hali ya mabadiliko ya tabia ya nchi.



Hivi karibuni mtandao huu umewatembelea wafugaji wa kijiji na kata ya rwabu kutaka kujua hali ya mifugo ambapo mwenyekiti wa kijiji hicho bwana Gelad Kuzenza,  alisema kuwa kwa makisio ya chini walikuwa na ng’ombe 1500 na lakini  kwa sasa wamebaki 700 huku akieleza kuwa  bei ya ng’ombe imeshuka hadi shilingi 15,000 huku wanunuzi wakisusia kununua mifugo hiyo wakati mwingine kutokana na hali ya ya kudhoofika zaidi.


Naye kwa upande wake Mwenyekiti wa chama cha wafugaji kanda ya ziwa kwa maana ya mikoa ya  Mara, simiyu shinyanga, mwanza geita na Kagera bwana Mrida mshota amekiri kuwepo kwa tatizo la mifugo mingi kufa kwa ukame na hasa ng’ombe ambapo amesema kuwa wameshaanza mikakati ya kukabiliana na tatizo hilo kwa kuanzisha mashamba ya majani kwa ajili ya mifugo yao.


Amesema zoezi hilo sio la muda mfupi kwa kuwa watanzania wengi na hasa mikoa ya kanda ya ziwa bado wanafuga ng’ombe wa kienyeji na wana mifugo mingi.


Amewataka wafugaji kuanza kubadilika kwa kufuga kisasa ili waweze kuendana na mabadiliko ya tabia ya nchi.



Post a Comment

karibu kwa maoni

 
Top