Mbunge
wa Arumeru Mashariki (Chadema), Joshua Nassari ameweka hadharani
ushahidi wa rushwa na waliopewa madiwani ambao wamejiuzulu Chadema kwa
madai ya kumuunga mkono Rais Magufuli.
Akizungumza
na waandishi wa habari leo, Nassari ambaye ameambatana na Mbunge wa
Arusha Mjini, Godbless Lema walitoa ushahidi huo na kueleza wataukabidhi
Takukuru na katika taasisi nyingine.
Katika
ushahidi wa video uliorekodiwa viongozi kadhaa wakiwema Mkuu wa Wilaya
ya Arumeru Alexander Mnyeti pamoja Mkurugenzi Mtendaji wa (H) Meru
Christopher Kazeri wamesikika wakiwashawishi madiwani kuhama na baadhi
waliahidiwa wangelipwa posho za vikao vyao vilivyobaki hadi 2020 na
kukamilishwa miradi yao.
Miongoni
mwa makubaliano hayo ni kuwa wapewe fedha na kupata ajira na
kukamilishwa miradi yote ya maendeleo waliyoahidi ikiwa ni pamoja na
wengine kubadilishiwa makazi pamoja na diwani mmoja kusaidiwa gharama za
kufanikisha harusi.
Hata
hivyo Mbunge Nassari pamoja na Godbless Lema wameahidi kesho watadfika
katika ofisi za TAKUKURU Dar es salaam kwa ajili ya kuukabidhi ushahidi
huo wa rushwa kwa Mkurugenzi Valentino Mlowola
Pamoja
na hayo wakati Nassari akiutoa ushahidi huo hadharani leo tayari
madiwani 10 wa Chama chake wameshapokelewa ndani ya CCM huku wengie
wakiwa wamepinga vikali kuhama chama hicho kwa sababu ya rushwa.
Aidha Nassari amesema ameamua kutoa ushahidi huo sasa kwa sababu alikuwa akiendelea kukusanya ushahidi wa kutosha.
Post a Comment
karibu kwa maoni