0
NA Gharos Riwa Bunda.

Kaimu meneja wa kampuni ya mount meru milas ambae pia ni mwenyekiti wa chama cha mapinduzi ccm wilaya ya Bunda Mheshimiwa Justine Rukaka Makongoro,amekabidhi tanki la maji la lita 2000 katika shule ya sekondari Nyiendo iliyoko katika Halmashauri ya Mji wa Bunda Mkoani  Mara.

Akikabidhi tanki hilo mheshimiwa Rukaka amesema kuwa kampuni ya Mount Meru Milas Ltd kwa kutambua changamoto ya maji katika halmashauri ya mji wa bunda na wilaya kwa ujumla imeamua kusaidia shule hiyo kwa kuwapelekea  tanki la maji litakalotumika kutunza maji kwa ajili ya matumizi mbalimbali kwa wanafunzi na waalimu.

Akipokea msaada huo Mwalimu mkuu wa shule hiyo Merida Maeda amesema wanaishukuru kampuni ya Mount Meru milas kuona umuhimu wa kuwapatia tanki hilo la kuhifadhia maji kwani wanakabiliwa na upungufu wa maji ukizingatia shule hiyo inawanafunzi wangi wapatao 1000.

Sambamba na hilo Mwalimu maeda amesema kuwa shule hiyo inachanzo cha maji kisichoaminika yaani kisima pamoja na maji ya mamlaka ya maji bunda BUWASA lakini wanashindwa kukidhi maitaji kutokana mamlaka kutokuwa na ratiba ya kueleweka katika usambazaji wa maji.

Hata hivyo kwa upande wao waalimu na wanafunzi shuleni hapo wameishukuru kampuni hiyo kwa  kuwapelekea tanki hilo,  na kusema kuwa awali halikuwepo na sasa litawasaidia katika shughuli mbalimbali za shuleni hapo. 

Post a Comment

karibu kwa maoni

 
Top