0
Mipango ya mkuu wa mkoa wa Arusha mrisho Gambo tangu aingie katika
mkoa huo kama mkuu wa mkoa imekuwa ikigusa hisia za wengi kwani imekuwa
ikiwalenga moja kwa moja wananchi haswa wale wa kipato cha chini katika
huduma mbalimbali za kijamii.

Licha ya kukutana na changamoto
nyingi zinazotokana na siasa amekuwa mstari wa mbele katika kusimamia
zaidi katika utendaji kwa kuzingatia kauli ya nchi kwa sasa inayoongozwa
na Rais John Pombe Magufuli kuwa "HAPA KAZI TU".

Mrisho Gambo
akizungumza na watumishi mbalimbali wa mkoa wa Arusha ameeleza kuwa kwa
sasa amedhamiria kuboresha zaidi huduma za afya kwa kuongeza Zahanati za
kisasa katika baadhi ya maeneo akianza na Moshono na Morombo ili
kuondoa msongamano wa wagonjwa katika hospitali ya mkoa Mount Meru na
kuongeza ufanisi katika kutoa huduma bora.

Post a Comment

karibu kwa maoni

 
Top