0

Sarah Msafiri mkuu wa wilaya ya Hanang akizungumza na wanakijiji wa Gendabi.
Zaidi ya wakazi 20’000  wa kata za Dawar na Gendabi wilayani Hanang mkoani Manyara wanaopata huduma ya maji kupitia mradi wa Halmashauri hiyo wamelalamikia zoezi la ukatwaji wa mita za maji unaofanywa na Halmashauri hiyo kutokana na viongozi wa kata hizo zenye makundi ya wafugaji na wakulima kuingia katika mgogoro wa kugombania maji na kusababisha uhasama wa kutoshirikiana.
Katika zoezi hilo,jumla ya vituo 51 katika kijiji cha Sebasi kilichopo kata ya Gendabi vinavyotiririsha maji kwenda katika kata ya Dawar vilikatwa na kusababisha mgogoro ulioingiliwa kati na kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya hiyo kutokana na wananchi wa kata ya Dawar kukesha nje kwa takribani mwezi mmoja wakipinga zoezi hilo.
Akizungumza na wakazi wa kata ya Dawar na Gendabi Mkuu wa Wilaya ya  Hanang’ Bi.Sarah Msafiri alisema kuwa ili kuepuka mgogoro huo kutoendelea ni lazima kuwepo na  utaratibu sahihi wa maji kwa watumiaji ili kuepuka lawama wanazotupiana kati yao ambapo kila kata imekuwa ikiwatuhumu  wenzao wanatumia maji vibaya.
Wakazi wa kata ya Gendabi wameelezwa kuwa wao ni walimaji wa mbogamoga ambazo zinahitaji maji   mengi kwa ajili ya kumwagiliwa  huku wakazi wa Dawar wakielezwa kuwa na mifungo mingi inayohitaji maji mengi  kwenye unyweshwaji
 ‘’Ninachotaka kuwaambia ni kitu kimoja tu  ndugu zangu ili mgogoro huu uishe kwanza ni lazima  mjue hiki ni kipindi cha kiangazi maji  huwa yanapungua siyo mengi kama kipindi cha masika,mnachotakiwa kukifanaya kwa sasa kwa kuwa gendabi mnalima  mbogamboga mnamwagilia  maji punguzeni ulimaji huo limeni kiasi kulingana  na upatikanaji wa maji’’alisema  Bi.Sarah

Wakazi  wa vijiji vya Gendabi na Dawari hutumia maji yananatokana na  chanzo  kilichokuwa katika kjiji cha Gendabi   kinachotoka mlima  Hanang.
Stephen Sulley ni diwani wa gendabi alieleza kuwa vijiji hivyo vinachangamoto ya kukosa mahusiano bora kati yao huku pia wanasiasa wakitumia tatizo la  ukosefu wa maji  kwa kuwarubuni wananchi  kuwekeana chuki baina yao.
 ‘’Mkuu wa wilaya  mimi naona  kata hizi mbili ni kama tunaoneshana ubabe tu kwa sababu  hapa siyo kwamba hakuna maji, maji yapo ila utaratibu unaotumika ndio mbovu sisi hawa jirani zetu Dawar tumewapa chanzo  cha maji wakitumie lakini bado wanatuona wabaya wanakuja kwetu na kukata mita zote za wanakijiji  sisi makosa yetu ni yapi?’’alisema Diwani Sulley.
Mkuu wa wilaya pia amevunja jumuiya ya maji iliyokuwepo kutokana na jumuiya hiyo kushindwa  kufanya kazi yake ambayo ni kusimamia mradi na kuripoti sehemu husika huku akitoa agizo kwa kata zote mbili kuunda jumuiya nyingine ndani ya wiki moja.

Post a Comment

karibu kwa maoni

 
Top