0
Diwani wa kata ya Mutuka Mheshimiwa Yona Wawo amesikitishwa na kitendo cha polisi kumuua kwa Bunduki mzazi mwenzake wakati wa mabishano ya kuhusu matumizi ya mtoto.
Tukio hilo lilitokea tarehe 27.10.2017 katika Bank ya Nmb tawi la Babati mkoani Manyara baada ya mwanamke huyo kumfuata mwezi wake ambaye ni askari Polisi wakati akiwa katika Lindo kwenye bank hiyo majira ya jioni saa 12:30.
Yona amesema anamfahamu vizuri mwanamke huyo kwani alikuwa ni mwanakijiji katika kata anayoingoza ya Mutuka hivyo ameguswa sana na kifo hicho na kuitaka mamlaka husika inayosimamia askari polisi iliangalie jambo hilo na kulikemea kwani inawatia hofu wananchi.

Post a Comment

karibu kwa maoni

 
Top