0
Image result for salimu mwalimu kinondoniMgombea Ubunge wa Jimbo la Kinondoni kupitia tiketi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Salum Mwalimu amedai hawezi kwenda Bungeni kuwa Mbunge wa CHADEMA bali yeye anataka kuwa Mbunge wa wananchi wote bila ya kujali vyama vyao. 
Salum Mwalimu ametoa kauli hiyo ikiwa yupo katika muendelezo wa kuomba kura kwa wananchi wa Jimbo la Kinondoni ambao wanatarajia kuingia katika chaguzi ndogo siku za hivi karibuni za kumtafuta Mbunge wanayemtaka katika Jimbo lao ambalo kwa sasa lipo wazi.
"Siendi kuwa Mbunge wa CHADEMA bali naenda kuwa Mbunge wa wananchi wa Kinondoni, nitakae watumikia kwa haki kila mmoja katika jimbo hili. Pia ni kwamba sitokubali kuwa sehemu ya wasaliti wala unafki",alisema Salum Mwalimu.
Aidha, Salum Mwalimu amesema anamatumaini tosha kuwa yeye ndio atakae kuwa Mbunge mtarajiwa wa Jimbo hilo huku akidai hatarajii kuona uchaguzi mdogo ukiwa unarudiwa kwa mara nyingine.
"Hatutarajii kuona uchaguzi mdogo mwingine hapa labda Mwenyezi Mungu aliyenipa uhai achukue pumzi zake lakini siyo vinginevyo", alisisitiza Salum.
Kwa upande mwingine, mgombea huyo amedai atatumia maarifa yake yote aliyonayo ili aweze kuwaunganisha wananchi wa jimbo hilo na kuweza kuzungumza pamoja katika kujenga maendeleo yao.

Post a Comment

karibu kwa maoni

 
Top