Ni katika kata za Uhamaka,
Mwankoko na Mtama ambako zoezi la Usajili Vitambulisho vya Taifa linaendelea
ambapo wananchi wa kata hizo wamejitokeza kwa wingi Kusajiliwa wakiamini kwa
wao kuwa na Vitambulisho vitawasaidia kupata huduma za Kijamii Kirahisi.
Mzee Asumani Said Mkazi wa
Kata ya Mwankoko anaeleza kwa yeye kuwa na Kitambulisho cha Taifa atanufaika na
huduma za Afya zinazotolewa na Serikali kwa wazee. 'Nimeamua kuchangamkia fursa hii
mapema nisije nikapitwa'
Huku
akiendelea kuhudumia wananchi waliofika katika Kata ya Mtama Kusajiliwa, Afisa
Msajili Mkoa Ndg. Catherine Makuri ambaye pia ni mratibu wa shughuli za Usajili
ngazi ya mkoa - Singida amesema katika mkoa wake wananchi wamejitokeza angalau
kwa idadi ya kuridhisha katika baadhi ya vituo vya Usajili ikizingatiwa ni
msimu wa kilimo ambapo wengi wanakuwa wako kwenye mashamba yao wakilima isipokuwa kata chache wananchi wananjitokeza
kwa Idadi isiyo ya kuridhisha na wengi kuja majira ya kuanzia Alasiri baada ya
kutoka kwenye kilimo. Zoezi la Usajili vitambulisho linaendelea katika wilaya
zingine za mkoa wa Singida: Ikungi na Mkalama.
Kwa wilaya ya Manyoni tumeshakamilisha zoezi la Usajili wa mkupuo na kwa
Iramba muda si mrefu zoezi litaendelea kwa awamu inayofuatia hivyo wananchi
waandae viambatanisho muhimu.
Naye
Mtendaji wa Kata ya Mwankoko Elias
Mulamuzi Kayungi anasema wanajitahidi
kutumia mbinu mbalimbali kufikisha ujumbe kwa wananchi ili wajitokeze kushiriki
zoezi litakalowawezesha kupata Kitambulisho cha Taifa. Ndg. Kayungi anatoa
rai kwa 'Hakikisheni Mnatumia fursa hii
Adhimu Kujisajili kwani wakati huu NIDA wanaendesha Usajili wa Mkupuo
ambapo huduma imesogezwa karibu na
makazi yenu iwapo hamtajitokeza itawagharimu kufika kwenye ofisi zao wilayani'.
Bi
catarina Fidel akiwa anapatiwa huduma ya Usajili hatua ya pili ya uchukuaji
alama za kibaiolojia katika Halmashauri ya Manispaa ya Singida.
|
Wananchi
wa Kata ya Mtamaa mkoani Singida katika foleni kuelekea kuchukuliwa alama za
kibaiolojia (Picha , Saini na Alama za vidole)
|
Post a Comment
karibu kwa maoni