Mabingwa watetezi wa ligi kuu soka Tanzania Bara Yanga wanaendelea
kuwakosa nyota wao muhimu kuelekea mchezo wao wa kesho dhidi ya Mwadui
FC.
Akiongea
leo mbele ya wanahabari msemaji wa timu hiyo Dismas Ten amesema
wachezaji watakao kosekana katika mchezo huo ni Donald Ngoma, Geofrey
Mwashiuya, Thabaan Kamusoko na Obrey Chirwa.
"Tunawachezaji wetu ambao bado ni wagonjwa na wataukosa mchezo wa kesho dhidi ya Mwadui huku Chirwa atakosekana kwasababu anatumikia adhabu ya kukosa mechi tatu aliyopewa na kamati ya maadili ya TFF'', amesema Ten.
Kwa upande wa mshambuliaji raia wa Burundi Amissi Tambwe, Ten amesema mchezaji huyo amepona Malaria iliyokuwa inamsumbua hivyo kinachosubiriwa ni uamuzi wa Mwalimu kama atampanga kesho.
Yanga inashika nafasi ya tano kwenye msimamo wa ligi ikiwa na alama 21. Mchezo huo wa kesho utachezwa saa 10:00 jioni kwenye uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam.

Post a Comment
karibu kwa maoni