0


Image result for KaMANDA SENGAMtu mmoja ambaye hajafahamika anaekadiriwa kuwa na umri wa miaka 30-40 amekutwa akiwa amekufa katika kijiji cha Haraa kata ya Bonga wilayani Babati Mkoani Manyara.

Mwili huo umegundulika jana katika kijiji hicho.

Kwa mujibu wa mwenyekiti wa kijiji cha Haraa John Bura Masawe ambaye ametoa taarifa hiyo amesema mwili huo waliukuta ukiwa tayari umeaharibika vibaya   huku Madaktari wakishauri uzikwe  katika eneo hilo kwa kuwa mwili ulishaanza kuharibika na haufai kubebwa.

Hata hivyo mwili huo umezikwa leo Februari 27.2.2018 katika kijiji hicho huku kukiwa hakuna taarifa zozote kutoka kwa ndugu au jamaa wa marehemu huyo.

 Kamanda wa polisi mkoa wa Manyara Agustino Senga amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kueleza kuwa 'inawezekana mtu huyo ameuawa sehemu nyingine na kuja kutupwa katika kijiji hicho.
Senga amewataka wananchi kushirikiana na jeshi la polisi kuweza kufichua wahalifu ili mkoa wa Manyara uzidi kuwa salama'.

Post a Comment

karibu kwa maoni

 
Top