0
Image result for chademaChama cha Demokrasia na Maendeleo [CHADEMA] Mkoa wa Manyara kimewashtumu vikali wakuu wa wilaya  na mkuu wa mkoa wa Manyara kwa kuwaweka ndani baadhi ya viongozi wa chama hicho na kauli wanazozitoa.
Akizungumza na WALTER HABARI mwenyekiti wa CHADEMA mkoa wa Manyara Lawrence Tara amesema hali hiyo inawafanya viongozi wa Chama hicho kufanya kazi kwa woga akieleza kuwa ni matumizi mabaya ya madaraka.
Wameyazungumza hayo wakiwa katika kikao chao cha baraza la viongozi mjini Babati.
Tara alisema January 12.2018 Mkuu wa wilaya ya Hanang Sarah Msafiri amewaweka ndani madiwani watatu kwa madai ya kushindwa  kuhamasisha maendeleo kwenye kata zao,amewataja madiwani waliokamatwa ni Peter Loy diwani wa Katesh mjini,Hashim Khamunga diwani wa Endasaki,Diwani wa kata ya Dirma Faustin Kamsinda na hivi karibuni amemtia ndani  mwenyekiti na diwani wa Basodesh Mchungaji Michael Boay.
Naye mwenyekiti wa Baraza la wanawake wa CHADEMA [BAWACHA] ambaye pia ni mbunge wa jimbo la Babati mjini mheshimiwa Paulina Philipo Gekul  amesema kuwa Mkuu wa mkoa ni mdogo kwa umri na hajui wajibu wake kwani anachokifanya inaonyesha wazi kuwa hajasoma katiba ya nchi inasema nini.
Amesema mkuu wa mkoa anafanya kazi za mkurugenzi na kazi ya katibu mwenezi wa Ccm mkoa.
Mkuu wa mkoa wa Manyara Alexander Mnyeti.
"Kwa hiyo mkuu wetu wa mkoa hafiti kabisa na hajui anachokifanya na mpaka sasa hajawahi kufanya kazi ya ukuu wa mkoa,sasa kama Rais atamuacha atapata majibu mapema sana, aliongeza Gekul.
Akiwa katika mkutano wa hadhara kata ya Haydom wilayani Mbulu juzi Januari 11.2018  Mkuu wa Mkoa wa Manyara,  Alexander Mnyeti aliwataka madiwani wa vyama vya upinzani kujiunga na CCM ili waweze kushirikiana naye kutekeleza ilani ya uchaguzi ya chama tawala.

Alisema yupo tayari kupokea simu ya diwani wa CCM hata akipigiwa usiku wa manane, ili kumpa msaada lakini si diwani kutoka vyama  vya upinzani.

Alisema diwani wa Chadema ni ngumu kufanikisha maendeleo ya wananchi kwa madai kuwa, hakuna ambaye atamsikiliza akiwasilisha hoja zake katika vikao vya halmashauri husika.

"Hata hapa Haydom najua ni ngome ya Chadema hata mwenyekiti wa kijiji namuona ana damu ya CCM, sasa ondokeni huko mje huku tutekeleze ilani ya uchaguzi ya CCM ya mwaka 2015 hadi 2020 kwa kuleta maendeleo," alisema Mnyeti.

Pia, aliwataka watumishi wa halmashauri hiyo kutekeleza na kufanikisha kwa vitendo ilani ya CCM hata kama hawana kadi ya chama hicho kwani ndicho ambacho kipo madarakani.
Ikumbukwe kuwa Mamlaka ya Mkuu wa Mkoa na Mkuu wa Wilaya kuagiza kukamatwa kwa mtu na kuwekwa rumande yako chini ya vifungu vya 7 (mamlaka ya mkuu wa mkoa) na 15 (mamlaka ya mkuu wa wilaya) vya Sheria ya Tawala za Mikoa, 1997. Vifungu hivyo vinafanana katika uandishi na hata mantiki isipokuwa tu maneno 'Mkuu wa Mkoa' na 'Mkuu wa Wilaya'.
Pia, kama Mkuu wa Mkoa au Wilaya ana sababu za kuamini kuwa mtu yeyote aweza kuvunja amani au kuharibu utulivu uliopo au kufanya kitendo chochote ambacho kinaweza kuvunja amani au kuharibu utulivu na uvunjifu huo hauwezi kuzuiwa kwa njia yoyote nyingine isipokuwa kumsweka rumande mtu huyo, Mkuu wa Mkoa au Wilaya aweza kuagiza kwa maneno au maandishi kukamatwa kwa mtu huyo.

Mtu aliyekamatwa kwa amri au maelekezo ya Mkuu wa Mkoa au Wilaya anapaswa kufikishwa mahakamani ndani ya saa 48 kwa ajili ya kufunguliwa mashtaka ya jinai. Endapo hatafikishwa Mahakamani kwa muda unaopaswa, na muda kuisha, anapaswa kuachiwa na hapaswi kukamatwa tena kwa amri ya Mkuu wa Mkoa au Wilaya kwa namna ile ile.

Wakati wa kuagiza kukamatwa kwa mtu yeyote au muda mfupi baada ya kuagiza, Mkuu wa Mkoa au Wilaya lazima aandike sababu za kukamata au kuagiza kukamatwa kwa mtu husika na kupeleka nakala kwa Hakimu ambaye mbele yake aliyekamatwa atafikishwa kwa ajili ya kushtakiwa.

Post a Comment

karibu kwa maoni

 
Top