0


Image result for chademaAliyekuwa Diwani wa kata ya Bagara Babati mjini mkoani Manyara kupirtia chama cha Demokrasia na Maendeleo [CHADEMA] Nichodem Bonifasi maarufu kama Nyeusi amejiunga na chama cha Mapinduzi.
Akitangaza kujiunga na Ccm leo Nyeusi amesema utendaji kazi wa rais John Pombe Magufuli uliotukuka ndio uliomfanya ajiunge na chama hicho huku akiahidi kuendelea kuunga mkono juhudi za Rais Magufuli katika kutekeleza ilani ya Chama cha Mapinduzi.
Aidha amesema bado anao uwezo wa kuwatetea wakazi wa kata ya Bagara na ameomba apewe ruksa kupitia chama cha mapinduzi na sio diwani wa Halmashauri ya mji wa Babati,  kufanya ziara na kumtangaza rais Magufuli.
Diwani huyo ameomba uongozi wa ccm umpatie ulinzi kwa maelezo kuwa kuna watu wanamfuatilia.
Naye katibu wa siasa na uenezi Ccm mkoa wa Manyara Jacob Aloyce Siay amesema jambo hilo la diwani huyo wa kata ya Bagara kujiunga CCM ni la kishujaa na la kupongezwa.
Kwa upande wake mwenyekiti wa vijana ccm mkoa wa Manyara Mosses Method Komba amesema wamempokea kwa mikono miwili diwani huyo.
Diwani huyo juzi katika baraza la madiwani linaloongozwa na Mwenyekiti Mohamedi Kibiki alionekana akiungana na madiwani wa Ccm katika sakata la kukikabidhi chama cha Mapinduzi Kituo cha Mabasi cha Babati.,madiwani wa Ccm walikataa suala kujadiliwa huku chadema wakitaka lijadiliwe.
Halmashauri ya mji wa Babati inaongozwa na wabunge wa Chadema ambao kwa idadi yao kwa sasa wapo wanne baada ya Diwani wa kata ya Bagara Nikodem Alfonsi kuondoka.

Post a Comment

karibu kwa maoni

 
Top