0


Image result for MGOMBEA SIHAAliyekuwa Mgombea Ubunge kupitia Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CDM) jimbo la Siha Mkoani Kilimanjaro Elvis Mosi amesema kuwa ana mpango wa kufungua kesi Mahakamani kupinga matokeo  ya uchaguzi yaliyompa ushindi Dr Godwin Molel wa CCM kwa madai kuwa taratibu na kanuni za uchaguzi zilikiukwa hivyo  anatarajia kulifikisha suala hilo Mahakamani.
Mosi ambaye alipata kura 5905 dhidi ya kura 25611 za Dr. Molel amesema, wanakusanya ushahidi wa kutosha ambao utaiwezesha Mahakama kutengua matokeo hayo na uchaguzi kurudiwa.
Akizungumza na waandishi wa habari nyumbani kwake Sanya Juu, Mosi amezitaja baadhi ya taratibu zilizokiukwa ni pamoja na kubadilisha matokeo ya kura zake katika vituo na kupewa Dr. Molel jambo ambalo lilimfanya asisaini fomu za matokeo.

Post a Comment

karibu kwa maoni

 
Top