0
Mbunge wa Rombo (CHADEMA), Joseph Selasini amemuomba Rais Magufuli kuruhusu Serikali kuweza kufanya semina na mafunzo kwa ajili ya kuwajengea uwezo baadhi ya Wakurugenzi wa halmshauri ambao utendaji wao umesababisha migogoro na watendaji wengine.
 
Selasini alisema hayo Februari 1, 2018 wakati akichangia Bungeni na kusema kuwa uwezo mdogo wa baadhi ya Wakurugenzi hao umekuwa tatizo na ndiyo maana wengine wamekuwa wakitafsiri vibaya agizo la Rais Magufuli kuhusu michango mashuleni.
"Ninaiomba Serikali iendelee kupitia uwezo wa Wakurugenzi wake na isaidie kuwapa uwezo ili waweze kusimamia shughuli za halmashauri vizuri vinginevyo tutapata shida na kazi hazitakwenda sawa sawa, baadhi ya halmshauri miradi ya maendeleo haisimamiwi vizuri. Hivi majuzi Mhe. Rais kwa nia nzuri kabisa ametoa maagizo kwamba michango mbalimbali ambayo haina tija katika shule iondolewe hichi saizi kimekuwa kilio cha Watanzania kutokana na uwezo mdogo wa Wakurugenzi"
Selasini aliendelea kusisitiza kuwa
"Na mimi nalisema hili ili Rais alisikie, uwezo mdogo wa Wakurugenzi umefanya wametafsiri agizo lile vibaya kwa sababu zipo halmshauri na wilaya ambazo wazazi katika kila shule walishakubaliana utaratibu wao namna watoto wao wanapopata chakula mashuleni na utaratibu huo hausiani na Mkuu wa Shule, Mkurugenzi bali wazazi wanachama chao na bajeti zao na wao ndiyo wanapanga watoto wale nini kwa hiyo watoto wamekuwa wakila shuleni. Mimi naelewa upo uhusino mkubwa wa tumbo na kichwa, mtoto ambaye hajashiba hawezi kuzingatia yale anayofundishwa sasa Wakurugenzi hao baadhi yao wamekuwa kama roboti wamekwenda kutengeneza majedwali na kuzuia wale wazazi ambao kwa nia nzuri kabisa walikuwa wanachanga chakula kwa ajili ya watoto wao" alisema Selasini.
Mbunge huyo alidai kitendo ambacho kinafanywa na baadhi ya Wakurugenzi ni kuibomoa serikali na si kuisaidia hasa zaidi kwenye maamuzi hayo yanayohusu sekta ya elimu kwani amedai kuwa katika jimbo la Rombo shule zote za msingi na sekondari watoto wamekuwa wakila shule na wazazi kupitia vyama vyao ndio wamekuwa wakiratibu mambo hayo lakini toka kauli ya Rais imetolewa jambo hilo limeleta shida.

Post a Comment

karibu kwa maoni

 
Top