0

Mkuu wa wilaya ya Babati Mheshimiwa Raymond Mushi akikabidhi mkataba huo kwa mkurugenzi wa BAWASA Mhandishi Iddy Yazidi Msuya.

Wanakijiji wa Nakwa kata ya Bagara mjini Babati kuanza kufurahia huduma za maji baada ya Halmashauri ya mji kuukabidhi mradi wa maji wenye thamani mya shilingi Milioni 806,575,730  kwa Mamlaka ya Maji  Safi na Usafi wa Mazingira Mjini Babati [BAWASA] hii  na kushuhudiwa na Mkuu wa Wilaya ya Babati Raymond Mushi na Mkurugenzi wa mji Fortunatus Fwema.

Mkurugenzi wa Bawasa Eng. Iddy Yazidi Msuya  amesema kuwa  Mradi huo umekabidhiwa katika mikono salama hivyo  wakazi wa Nakwa wanaopata shida ya Maji kwa muda mrefu wategemee huduma safi za maji saa 24.

Amewaeleza wakazi hao kuwa wataanza kufurahia huduma za BAWASA ndani ya wiki mbili baada ya kukagua na kuyatazama yale maeneo korofi katika upatikanaji wa maji.
Eng. Msuya amesema jukumu lao ni kuhakikisha wakazi wa Nakwa wanapata maji hivyo wananchi watoe ushirikiano katika kutunza miundo mbinu iliyopo na kutoa taarifa pindi wanapoona bomba linavuja.
Mkuu wa wilaya ya Babati Eng.Raymond Mushi akizungumza na wakazi wa Nakwa.

Mradi huu wa maji  uliotekelezwa na Halmashauri ya Mji wa Babati  na serikali kuu  pamoja na  bank ya dunia [WB] ulianza kutekelezwa Novemba22  Mwaka 2013 na kukamilika July 26 Mwaka 2017.

Aidha mradi huo unawahudumia wakazi wa Nakwa wapatao 6,688 chenye vitongoji vitano vyaa Sumbi Kayto,Magara,Mageni na Simbay.

Mpaka kukamilika kwa mradi huu imetumika shilingi Milioni 806,575,730 kutoka serikali kuu na shilingi  Mlioni 5 nguvu za wananchi.

Mkuu wa wilaya ya Babati Raymond Mushi ameeleza kuwa aliukagua mradi huo vizuri kwa kushirikana na mkurugenzi wa BAWASA Eng. Iddy Yazidi pamoja na mkurugenzi wa mji wa Babati Fortunatus Fwema na kumuagiza mkandarasi kurekebisha kasoro zilizopo katika mradi huo.

Mkuu wa wilaya  akiongozana na wataalamu wa maji alitembea kwa miguu Kilometa 37 kukagua kasoro zilizopo katika mradi huo huku akiwapongeza wananchi waliogundua kasoro kwenye mradi huo.

Kwa upande wake mkuu wa wilaya ya Babati Raymond Mushi amesema kuwa mradi huo kwa awamu ya kwanza  ulikumbwa na harufu ya ufisadi na kwa sasa Taasisi ya Kuzuia na kupambana na Rushwa [TAKUKURU] inaendelea na uchunguzi hivyo wananchi watoe ushirikiano pindi wanapohitajika kutoa ushahidi na taasisi hiyo.

Post a Comment

karibu kwa maoni

 
Top