JESHI
la Polisi mkoani Mwanza kwa kushirikiana na Taasisi ya Kuzuia na
Kupambana na Rushwa Tanzania (TAKUKURU) mkoani hapa imemkamata
Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Misungwi Bw. Anthony Bahebe.
Pia
Mwanasheria wa Halmashauri hiyo Bw. Alphonce Sebukoto naye amekamatwa
na Jeshi hilo. Viongozi wote hao wanakabiliwa na tuhuma za matumizi
mabaya ya madaraka na ubadhilifu wa fedha za umma.
Akizungumza
na waandishi wa habari, Kamanda wa Polisi wa mkoa wa Mwanza, Ahmed
Msangi alisema kukamatwa kwa viongozi hao kunatokana na tuhuma
mbalimbali zinazowakabili ikiwa ni pamoja na matumizi mabaya ya
madaraka.
Kamanda
Msangi alisema, Bw. Sebukoto alikamatwa Februari 19, 2017 na Bw. Bahebe
amekamatwa leo na wote wanaendelea kuhojiwa na Polisi kwa kushirikiana
na TAKUKURU.
Naye
Kamanda wa TAKUKURU wa mkoa wa Mwanza Mhandisi Ernest Makale alisema
Bw. Sebukoto aliidhinisha malipo ya sh.milioni 278 zilipwe katika
akaunti binafsi ya Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo Bw. Bahebe.
Alisema
Bw. Sebukoto aliidhinisha malipo hayo kwa Bw. Bahebe Novemba 2017
wakati alipokuwa anakaimu nafasi ya ukurugenzi wa Halmashauri ya
Misungwi ambapo jumla sh. milioni 138 ziliingizwa katika akaunti binafsi
ya Mwenyekiti huyo. Alisema kiasi kingine cha fedha kinachunguzwa
kubaini kilipo.
Kukamatwa
kwa viongozi hao kunatokana na juhudi za Serikali katika mapambado
dhidi ya matumizi mabaya ya madaraka pamoja na fedha za umma.
Februari
19, 2019 akiwa katika ziara yake wilayani Misungwi Waziri Mkuu Kassim
Majaliwa alimsimamisha kazi Mwanasheria wa Halmashauri ya wilaya ya
Misungwi Bw. Sebukoto na kuagiza achungunzwe na vyombo husika.
Alichukua
hatua hiyo baada Mwanasheria huyo kushindwa kutekeleza majukumu yake
ipasavyo ikiwa ni pamoja na kushindwa kuishauri vyema halmashauri hiyo
na kuisababishia hasara ya sh. milioni 278.
Amesema
Mwanasheria huyo Novemba 2017 wakati alipokuwa anakaimu nafasi ya
ukurugenzi aliidhinisha malipo ya sh.milioni 278 zilipwe katika akaunti
binafsi ya Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo Bw. Anthony Bahebe.
Waziri
Mkuu alisema Bw. Bahebe aliishtaki halmashauri hiyo akidai kulipwa
fedha kwa ajili ya kazi ya ukandarasi wa mradi wa maji Igenge uliojengwa
na kampuni ya ukandarasi ya Seekevim.
Alisema
mradi huo ulianza 2014 na ulitakiwa ukamilike 2015. Mwanasheria huyo
aliidhinisha malipo hayo wakati ambao tayari hati maalumu ya uwakilishi
ilikuwa imekwisha tangu Desemba 2015.
Alisema
Mwanasheria alimlipa Mwenyekiti wa Halmashauri kwa kufanya kazi na
Halmashauri jambo ambalo ni kinyume na maadili ya utumishi wa umma.
Hivyo
alitumia fursa hiyo kuwakumbusha watumishi wa umma kuzingatia maadili
ya utumishi na matakwa ya kisheria katika utekelezaji wa majukumu yao.
Post a Comment
karibu kwa maoni