0


Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Tulia
Ackson amesema hawezi kumzungumzia au kumshauri Mange Kimambi kwani hana
uhakika kama ni binadamu wa kawaida.

Dkt. Tulia alisema kuwa hawezi kumshauri kitu mwanamke huyo maarufu
kwenye mitandao ya kijamii kwani kwa kile anachosikia kuhusu
anachokifanya mitandaoni ana mashaka ‘ni aina gani ya kiumbe wa
binadamu’.

“Sina hakika kama yeye ni binadamu wa kawaida kama mimi kwa hiyo
sijui labda nikikutana naye ndiyo nitajua kitu cha kuzungumza naye,”
alisema.


“Lakini kwa yale nayoyasikia hapa na pale sina hakika kama yeye ni
binadamu wa kawaida kama mimi ila kama yupo kama mimi basi nitapata
fursa ya kumshauri nikionana naye,” aliongeza.


Aidha, Dkt. Tulia alisema kuwa hawezi kusema kama anachokifanya
anakosea au yuko sahihi kwani inategemea yeye ni jamii gani ya binadamu
(specie).

“Huenda hakosei, labda ni aina yake ya binadamu yaani ni specie tofauti.
Hivyo, kama yeye ni specie ya tofauti huwezi kusema anakosea,” Dkt.
Tulia anakaririwa.



Post a Comment

karibu kwa maoni

 
Top