0
Mbunge Mahawe akikabidhi jezi pea mbili kwa vijana wa kata ya Bagara.


Nbunge Ester Mahawe akikabidhi jezi kwa viongozi chama cha Mapinduzi kata ya Bagara.
Mbunge wa Mkoa wa Manyara [CCM] Ester Alexeander  Mahawe amewahimiza vijana kujikita zaidi katika michezo kwani ni ajira pia kuweka afya zao safi.

Ametoa kauli hiyo alipokuwa anawakabidhi jezi seti mbili za rangi ya wapinzani wa Jadi Tanzania Simba na Yanga Nyekundu na Njano vijana wa Chama cha Mapinduzi kata ya Bagara mjini Babati.

Pamoja na jezi hizo pia ametoa mipira miwili ya kisas baada ya mwenyekiti wa mtaa huo kuomba kwa Mbunge huyo hivi karibuni jezi na mipira kwa ajili ya kuandaa timu ya mpira wa miguu ya Kata ya Bagara.

Akizungumzia mchezo wa Netball Mahawe amesema kwa kuwa yeye alikuaga mchezaji wa mchezo huo atahakikisha mchezo huo kwa wanawake unakuwepo mbele Babati na mkoa wa Manyara kwa ujumla huku akiwataka wasichana nao wasibaki nyuma katika michezo.

Post a Comment

karibu kwa maoni

 
Top